ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 12, 2011

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Ubalozi wa Tanzania Washington, DC unawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kazi zilizotangazwa hapa chini. Ubalozi wa Tanzania Washington, DC unazingatia usawa wa kijinsia katika kutoa ajira. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

1.   KATIBU MAHSUSI (SECRETARY/ADMINISTRATIVE ASSISTANT) : NAFASI 1

KAZI ZA KUFANYA

                             i.        Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida ;
                            ii.        Kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa ;
                           iii.        Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika;
                           iv.        Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi Ubalozini;
                            v.        Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa Maafisa wengine na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na Maafisa hao;
                           vi.        Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maafisa husika na kukusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika ;
                         vii.        Kutunza taarifa/kumbukumbu za hesabu (Accounts payable/ receivable) ; na
                        viii.        Kazi nyingine atakazopangiwa.


SIFA ZA MWOMBAJI

                             i.        Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kuendelea na kuhudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani husika (‘High School graduates and above who have basic office skills and 1-2 years typing programs in Office Administration).
                            ii.        Awe anafahamu lugha ya Kiswahili na Kiingereza na awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail, Excel, Power point na Publisher.


SIFA ZA ZIADA
Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.



2.   MPOKEZI (RECEPTIONIST/CUSTOMER CARE) : NAFASI 1

KAZI ZA KUFANYA

                             i.        Kupokea wageni na kuwasaili shida zao;
                            ii.        Kutunza jesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kkutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni;
                           iii.        Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani;
                           iv.        Kupokea simu kutoka nje  na kuzisambaza kwa maafisa husika;
                            v.        Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma;
                           vi.        Kuhakikisha kwamba wageni wageni wanaoingia ndani wana miadi (Appointment) au wamepata idhini ya maafisa husika ;
                         vii.        Kujibu hoja mbalimbali zinazoulizwa na wageni/wateja wa Ubalozi na kutoa taarifa kwa umma kuhusu huduma zinazotolewa na Ubalozi ; na
                        viii.        Kazi nyingine atakazopangiwa.


SIFA ZA MWOMBAJI

                           iii.        Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kuendelea na kuhudhuria Mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu na kufaulu mtihani husika (‘High School graduates and above who have Good interpersonal and Customer Service Skills)
                           iv.        Awe anafahamu lugha ya Kiswahili na Kiingereza na awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail, Excel, Power point na Publisher.


SIFA ZA ZIADA
Awe mwenye uwezo wa kuzungumza lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kireno, Kirusi, Kichina, Kijerumani, Kihispania na Kiarabu.



MASHARTI KWA WAOMBAJI WOTE :-

1)   Maombi yaandikwe na kuambatanishwa nakala za vyeti vya Shule, Vyuo, Vyuo Vikuu (Certificate and transcript) na kozi ulizohudhuria.
2)   Wasifu binafsi wa mwombaji (CV).
3)   Waombaji wawe wakazi halali wa Marekani wenye vibali vya kufanya kazi (Legal Immigrant/Permanent Resident with valid working permit).
4)   Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi yote ni Aprili 22, 2011.
Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

AMBASSADOR
THE EMBASSY OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
1232 22ND STREET, N.W.
WASHINGTON, D.C. 20037.

No comments: