ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 13, 2011

KIBARUA AJERUHIWA AKISHUSHA VIOO GARINI NA BAADAE AFARIKI DUNIA!

Shabani Dede akiokolewa na wananchi baada ya kutumbukia kwenye boksi la vioo alilokuwa akilishusha kwenye lori aina ya Isuzu.
NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Shabani Dede jana mchana alijeruhiwa vibaya baada ya kutumbukia kwenye boksi la vioo alilokuwa akilishusha kwenye lori aina ya Isuzu namba za usajiri T603 AGG ili kuviingiza kwenye duka la mfanyabiasha mwenye asili ya Kiasia, Mtaa wa Mlapakolo, jirani na Hotel ya Mount Uluguru ambapo alifunikwa na vioo hivyo na vingine vikimkata sehemu mbali mbali za mwili wake.


Mtandao huu ulimshuhudia mmiliki wa duka hilo ambaye kwa ‘ubize’ wa tukio hilo hakuweza kuzungumzia tukio hilo kwani aliamua mara moja kuomba msaada kwa wananchi waliofurika katika eneo hilo walivunje boksi  hilo pamoja na vioo hivyo kwa lengo la kumchomoa majerehi huyo.

Wananchi walimtoa kijana huyo akiwa ameshapoteza fahamu kufuatia kukatwa na vioo na kukosa hewa kwa muda aliokuwa amefunikwa na vioo hivyo.

Mwandishi wetu alizungumza na rafiki wa Dede aitwaye Dago Awadh ambaye alisema: "Mimi na Dede tulikodiwa na Mhindi huyo kumshushia mzigo wake huu na kwamba wakati tukihangaika,  lori moja lilipita jirani ya Fuso hili hivyo mtikiso wake ulisababisha boksi hili kuyumba na Dede alipojaribu kujiokoa alitumbukia ndani na kujeruhiwa kama ulivyoona, " alisema Awadh.

Baada ya Dede kuchomolewa kwenye boksi hilo alikimbizwa hospitali na teksi iliyokodiwa na mwenye mali ambaye naye aliwasha gari lake na kueleka hospitalini.

AMEFARIKI:
HABARI za kuhuzunisha zilizotufikia baadae ni kwamba Shabani Dede aliyetumbukia kwenye boksi la vioo jana, amefariki dunia leo alfajiri katika hospital ya mkoa wa Morogoro alikokuwa amelazwa. Majira ya saa nne asubuhi, mtandao huu ulifika katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa lengo la kumjulia hali na kuzungumza naye kuhusiana na janga hilo lililomkuta jana,kwa huzuni kubwa baadhi ya wauguzi wa hospita hiyo waliueleza mtando huu kwamba kijna huyo alifariki leo alfaji.

CHANZO:GPL

No comments: