Raia akipata kikombe cha Babu Ambilikile Mwasapile wa Loliondo
WAKATI baadhi ya viongozi mbalimbali wa dini wakibeza tiba ya magonjwa sugu inayotelewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila katika Kijiji cha Samunge, Askofu wa Kanisa la Anglikana, Jimbo la Dayosisi ya Kati, Godfrey Mhogolo amesema dawa hiyo ni mkombozi wa afya za watu na inatetea uwezo wa Mungu.
Alisema hayo jana katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, mjini Dodoma.
Akifafanua kwenye tafakari ya ujumbe wa siku hiyo kuu alisema, uroho wa fedha walizokuwa wanapa kwa kile alichosema “wanajuza neno la Mungu” sasa umedhoofishwa kwa nguvu ya Mungu ya kikombe cha dawa ya miti iliyojidhihirisha kwa Mchungaji huyo Samunge na kuokoa mamia ya afya za watu baada ya shetani kutesa afya zao kwa muda mrefu. Namshukuru sana Babu kwa kazi anayofanya na ninaahidi kumwombea kila siku.”

Alisema dawa hiyo ni moja ya kazi ya Mungu aliyoifanya wakati wa uumbaji wa dunia akifafanua kuwa aliweka miti ya aina mbalimbali kwa matumizi tofauti akitolea mfano wa moja ya kazi hiyo kuwa ni kikombe cha Babu.
Alisema hata dawa za hospitali zinazofanyiwa utafiti na wazungu na kutumika kwa wanadamu wote ulimwenguni zimetokana na miti aliyoiumba Mungu.
Huku Samunge, Serikali imesitisha safari za ndege zilizokuwa zikiendelea kupeleka wagonjwa katika kijiji hicho kupata tiba.
Ndege hizo kutoka sehemu mbalimbali nchini zilikuwa zikiendelea kutua katika Uwanja wa Wasso uliopo kilometa takriban nane kutoka mjini Loliondo, licha ya Mchungaji Mwasapila kusitisha utoaji wa dawa ya magonjwa sugu wakati wa Sikukuu za Pasaka.
Taarifa zinasema kuwa uamuzi wa Serikali kuzuia ndege ulitangazwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alipofanya ziara katika uwanja huo.
Msimamizi wa Uwanja wa Wasso, Gabriel Masare aliliambia Mwananchi kuwa Lali alilazimika kufika uwanjani hapo, kutoa maelekezo ya kusitishwa safari za kwenda Samunge baada ya ndege tatu kutua zikiwa na wagonjwa.
Masare alisema baada ya ndege kutua juzi Alhamisi, mkuu huyo wa wilaya alifika na kuwataka wasiendelee kupokea ndege zinazopeleka wagonjwa Samunge kama ambavyo tayari Serikali mkoani humo, ilivyotangaza kusitisha safari hizo.
"Tulikuwa hatujapa maelekezo ya kuzuia ndege, ila sasa tumezuia hadi Jumanne kama ambavyo Serikali imeagiza," alisema Masare.
Wakati safari za ndege zikisitishwa, uwanja huo umeanza kufanyiwa ukarabati kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji.
Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia wafanyakazi wa muda wa uwanja huo, wakifyeka nyasi huku wengine wakisafisha mazingira ya uwanja.
Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia wafanyakazi wa muda wa uwanja huo, wakifyeka nyasi huku wengine wakisafisha mazingira ya uwanja.
Masare alisema ukarabati huo unaofanywa ni wa kawaida ili kuboresha mazingira.
Awali, uwanja huo ulikuwa ukipokea wastani wa ndege moja kwa wiki, lakini tangu Mchungaji Mwasapila aanze kutoa matibabu ya magonjwa sugu katika Kijiji cha Samunge, umekuwa ukipokea wastani wa ndege tano kwa siku.

Kwa mujibu wa Masare, changamoto kadhaa zinaukabili uwanja huo ikiwa ni pamoja na kukosa chumba cha kupumzikia abiria, maji, umeme na huduma ya vyakula na vinywaji.
Bei ya bidhaa juu tena Samunge
Bei za bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula na vinjwaji imeongezeka tena Samunge kutokana na ongezeko la watu wanaosubiri kupata tiba kijijini hapo.
Bei ya bidhaa juu tena Samunge
Bei za bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula na vinjwaji imeongezeka tena Samunge kutokana na ongezeko la watu wanaosubiri kupata tiba kijijini hapo.
Hivi sasa, chupa moja ya maji makubwa ya kunywa imerejea kuuzwa kwa Sh2,000 badala ya Sh1,000, huku chupa ndogo ikiuzwa Sh1,000 badala ya Sh500.
Bei ya vyakula na nyama pia imepaa. Sasa sahani moja ni kati ya Sh2,500 na 3,500 tofauti na awali ambapo ilishuka hadi kati ya Sh1,000 na 2,000.
Ongezeko hilo pia limekumba mawasiliano. Vocha za simu zinazotakiwa kuuzwa Sh500 zinauzwa 600 na za Sh1,000 zinauzwa 1,200 huku vocha za Sh2,000 zikiuzwa kwa Sh2400.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila ametangaza kuwa ataanza tena kutoa huduma ya dawa ya kikombe Jumatatu ya Pasaka.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila ametangaza kuwa ataanza tena kutoa huduma ya dawa ya kikombe Jumatatu ya Pasaka.
Akizungumza na Mwananchi jana, msaidizi wake, Fred Nisajile alisema kuwa baada ya Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka huduma hiyo kusitishwa, Jumatatu itaendelea kutolewa kama kawaida.
Hata hivyo, aliwataka watu wanaotaka kwenda kupata tiba ya Mchungaji Mwasapila Samunge kufuata maelekezo ya Serikali ili kuepusha usumbufu.
"Kama unavyoona, hapa shida ambayo leo (jana) wanapata hawa watu ni kupuuza maagizo ya Serikali ya kusitishwa safari za kuja huku, hadi baada ya Sikukuu," alisema Nisajile.
Jana, baadhi ya watu hasa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kenya walikuwa wamekaa bila kupata kikombe kutokana na kusitishwa kutolewa kwa huduma hiyo.
Mamia ya watu kutoka ndani na nje ya nchi, bado wanafurika Samunge, kupata tiba ya magonjwa mbalimbali kama pumu, Ukimwi, kisukari, kansa, vidonda vya tumbo na mengine.
Tayari wananchi kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uingereza, Sweden, Uholanzi, Falme za Kiarabu, Lebanon, Marekani wameshatua Samunge kupata tiba.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment