ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 12, 2011

Ligi ya Africa,Houston,GHANA HOI

Na Juma Maswanya
Kwa mara nyingine tena timu yetu Tanzania (d-squad) imeendeleza dozi kwenye ligi ya mataifa ya Afrika huku safari hii zoruba likiikumba Ghana baada ya kupokea kipigo cha magoli 3-2.Kipigo kama hicho kilitolewa wkd iliyopita kwa Liberia ingawa safari hii kilitolewa kwa staili ya tofauti zaidi. Zikiwa zimesalia dakika chini ya 20 mpira uishe timu yetu ilikuwa chini kwa mabao 2-1 na hapo ililazimika kufanya "extra work" kusawazisha na hatimaye kuongeza bao la ushindi,hali iliyowafanya Ghana washangae wasielewe kilichotokea.
 
Mpaka half time timu zote zilitoshana nguvu kwa kumaliza bila kufungana ingawa tulikaribia kupata goli kwa mpira wa kichwa uliopigwa na Fahad kugonga mwamba wa juu.Kipindi cha pili Tanzania walianzisha shangwe kupitia kwa Ally Ndikumana aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18 na mpira kumpita kipa kabla ya kujaa wavuni.Winga huyo wa kushoto alionyesha uhai mkubwa katika ubavu wa kushoto na ndio aliyetengeneza bao la ushindi.
 
Ghana walisawazisha na dakika chache zilizofuata waliandika bao la pili na kuipa timu yetu kazi kubwa ktk kutafuata ushindi.Tanzania tulipata goli la kusawazisha kwa penati iliyotolewa na mwamuzi mara baada ya Bittebo kuchezewa faulo ndani ya box.Penati hiyo muhimu ilifungwa na Kwame na kuamsha burudani tena.
 
Kuingizwa kwa Alune na Moody waliochezeshwa kama viungo washambuliaji kuliizidishia uhai timu yetu kwenye eneo hilo na kutengeneza mashambulizi zaidi ambapo safari hii Moody ndiye aliyerudisha shangwe kwa timu yetu baada ya kuipatia Tanzania goli la ushindi huku dakika zikiwa zimesalia chache mpira kuisha.
 
Moody(baba ayubu) alifunga goli hilo kwa shuti kali kutokea wingi ya kulia baada ya Ndikumana na Ally kumtengenezea mpira huo.Pia kurudi kwa kiungo mkabaji Ignas kuliisadia sana timu yetu ambapo ktk mechi hiyo alikuwa nguzo muhimu.
 
Safu ya ulinzi kama kawaida ilikuwa imara chini ya Charle mavuno aliyesaidiana na Fahad huku pembeni wakicheza Walter na Godfrey. Golini alisimama John aliyecheza vizuri na kuoka baadhi ya michomo hatari.
 
Mechi hiyo pia ilivutia mashabiki wengi wa mataifa mbalimbali waliokuwa na hamu ya kutaka kujua kwanini timu yetu Tanzania inashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ngumu inayoshirikisha timu 10 mwaka huu.Ni wazi kuwa ushindi wetu wa jana ulizidi kuzifanya timu zingine kuingia wasiwasi wa kukumbana na timu yetu jambo linaloashiria kuwa mechi zinazokuja zinaweza kuwa ngumu au kuwa nyepesi zaidi kwa upande wetu.
 
Ushindi huo bado unaibakiza timu yetu katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ambapo Cameroon wanaongoza kwa kutuzidi sisi kwa goal difference japo wote tuna point kumi huku pia kila timu ikiwa imebakiza michezo mitano kabla ya ligi kumalizika.
 
Matokeo ya mechi zingine za jana yalikuwa;
                                                       Nigeria 0-0 Sudan(2)
                                                       Angola 1-4 Cameroon
                                                       Congo 4-0 Ivory Coast
                                                    Sudan(1) 0-2 Liberia
Msimamo wa ligi mpaka sasa ni; 
             

Kikosi kilikuwa;
John Kijan(kipa), Walter,Godfrey,Fahad,Charles mavuno,Andrew/Kwame/Ignas,Sekulu/Bittebo/Moody,Abduli/Alune,Steve(Capt wa mchezo),Ally Mtumwa,Cassius/Ally Ndikumana.
Wachezaji wa Akiba;
Shaibu,Twahiru,Hamis Mulla.
Majeruhi;
Victor Vedasto (hamstring)
Tom (sprained finger)
James Luhanga (muscle pull)
Viongozi;
Juma Maswanya (Head coach),Himidy(Assisant coach),Jenga Ngalawa,Allan Mphuru, Arthur Mneney.
 
 Mechi yetu inayofuata;
 
TANZANIA vs SUDAN 2 (mechi kuanza saa 11:30 jioni JUMAMOSI tarehe 16 April 2011 kulekule Eldridge park)
 
Kutokana na mechi hii kuwa jumamosi,tunategemea kufanya mazoezi ya mwisho ijumaa hii pale Harwin kuanzia saa 11:00 jioni huku kila mmoja kwa muda wake akiendelea na mazoezi binafsi katikati ya wiki.
 
d-squad pamoja

1 comment:

Anonymous said...

hiii timu inaonekana ina beki mbovu sana so mjitahid katika beki...pia mchezaj wenu rahim yuko wapi na mbona mnamuweka huyo kijana hamis mulla benchi wakat mimi niliuona minessota kuwa ni mwiba kwa mabeki!!?? Sina mengi nawatakia kila la kheri@ mdau toka Minneapolis,minnesota!!!