Hamfrey Owen mchezaji wa Simba
Saleh Mohammed shabiki wa Yanga
Ushabiki wa Yanga na Simba kutambiana kila mtu akivutia kwake kwamba ushindi ni lazima hii ndio kawaida miamba hii miwili inapokaribia kuumana majigambo ya mashabiki na miongoni ya wachezaji hua si ya kawaida.
Mtanage huu uliopamgwa kuchezewa Columbus,Ohio utakuwa ndio mtanange wa kwanza kuzikutanisha Simba na Yanga nje ya DC na hii itakua mechi ya kwanza mwaka huu ambayo imepangwa kuchezewa wanja la Whitestone Park of Roses 3923 North High Street,Columbus,OH,43214-3335,Siku ya Jumapili May 29,2011 saa 4:30 jioni.
Mechi hii ya Columbus,ni ya Simba kujaribu kulipiza kisasi baada ya mwaka jana kufungwa mechi zote mbili.
Mechi ya marudiano mwaka huu imepangwa kufanyika siku ya sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wetu zitakazo fanyikia DC.
Kepteni wa Simba Libe Mwang;ombe anawaomba wachezaji wote wa Simba popote pale mlipo Mjiweke fiti na mkija Columbus njoo na vifaa lakini lazima uwe fiti mechi hizi si lelemama,alionya.
Kwa upande wa Yanga Timu Kepteni Adam Jongo yeye hakutaka kusema mengi zaidi ya kutania tu kwamba safari hiii Simba watafute pakutokea niko fiti kupita kiasi winter yote mimi nilikua nafanya mazoezi nae akawaomba wachezaji wa Yanga wote popote pale mlipo mje mkiwa fiti,Columbus Mashabiki wa Yanga kaeni mkao wa kula na akaongezea Midfield yake Aris ameisha aanza mazoezi mepesi anategemea ikifika May 15 atamjaribu kwenye mechi ya majaribio lakini yote inategemea Daktari atakavyoshauri.
Mashabiki wote Columbus,Ohio na Vitongoji vyake wanausubiri kwa hamu mpambano huu wa kukata na shoka ambao Simba wamesema kufungwa kwao mwiko.
No comments:
Post a Comment