Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
MGOGORO mkubwa wa kugombea mapato ya magari yanayokwenda kupeleka wagonjwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila, umeibuka baina ya Serikali ya Kijiji cha Samunge na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.Mgogoro huo ulianza Aprili Mosi, mwaka huu, baada ya halmashauri hiyo kuanza kutekeleza maagizo mbalimbali ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yanayoitaka ikusanye fedha zote zinazotokana na ushuru wa magari.

Tangu kuanza kwa utozaji wa fedha kwa magari yanayoingia Samunge, halmashauri ya kijiji hicho ndiyo iliyokuwa ikisimamia mapato lakini kwa kutumia vitabu vya stakabadhi za Halmashauri ya Wilaya.
Utaratibu huo mpya ni matokeo ya uamuzi wa pamoja baina ya wadau mbalimbali na baadhi ya wakuu wa mikoa waliokuwa wakijadili njia bora za uratibu wa magari yanayowapeleka watu Samunge, uliofanywa chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Akizungumza na timu ya waandishi wa habari wa Mwananchi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro, Dominick Lusasi alisema kutokana na maagizo ya ngazi za juu, waliamua kupeleka wataalamu kukusanya mapato ya magari.
Katika utaratibu wa awali, uongozi wa Kijiji cha cha Samunge ulikuwa ukitoza ushuru wa Sh2,000 kwa magari yanayochukua abiria kati ya mmoja na 12 na Sh5,000 kwa magari ya abiria 13 hadi 30 na Sh10,000 kwa magari yenye uwezo wa kuchukua zaidi ya abiria 30 wakati kila helikopta inayotua inatozwa kiasi cha Sh150,000.
Hesabu za Halmashauri ya Ngorongoro zinaonyesha kuwa tangu vilipoanza kutumika vitabu vya stakabadhi za halmashauri, fedha zilizokusanywa kati ya Machi 7 na 28, mwaka huu ni kiasi cha Sh15 milioni, na kwamba wastani wa mapato hayo kwa siku ni kati ya Sh800,000 na Sh1 milioni.
Utaratibu mpya
Kwa mujibu wa Lusasi, mchakato mpya wa kuangalia mfumo mzima wa usimamizi wa mapato na taratibu nyingine za utoaji wa tiba, umetangazwa na maelekezo kutoka serikalini yalitaka kila gari litozwe Sh5000 bila kujali aina wala ukubwa wa gari husika, wakati helikopta zitaendelea kutozwa Sh150,000.
Kadhalika, katika utaratibu huo ulioanza kutekelezwa Aprili Mosi, mwaka huu, Halmashauri ya Ngorongoro ndiyo iliyopewa jukumu la kukusanya mapato hayo na kati ya Sh5,000 na Sh3,000 zinatakiwa kubaki Serikali Kuu na Sh2,000 ndizo zinazobaki halmashauri kwa ajili ya kugharimia shughuli za usafi katika maeneo husika.
"Kikao hicho cha wakuu wa mikoa na Waziri Lukuvi walikubaliana halmashauri baada ya kukusanya fedha sehemu ya fedha itapelekwa ofisi za mikoa ili kuhudumia vituo vya kupitisha wagonjwa ambavyo tayari vimetengwa," alisema Lusasi.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo alikiri kwamba wameshindwa kuanza kukusanya fedha hizo kama walivyoelekezwa, kutokana na kuzuka vurugu baina ya wakusanya ushuru wa kijiji na wale wa halmashauri hasa baada ya uongozi wa kijiji kung'ang'ania kuendelea kukusanya mapato hayo.
"Kutokana na hali hii tunatarajia kufanya kikao baina yetu, uongozi wa kijiji na ofisi ya mkuu wa wilaya ili kuona ni jinsi gani tutatatua mgogoro huu ili makusanyo ya halmashauri yaanze," alisema.
Awali, Diwani wa Kata ya Samunge, Jackson Sandea alisema, kijiji kina haki zote za kukusanya mapato yote kwani fedha ambazo zinakusanywa zinatumika katika masuala ya usafi, afya na kutunza mazingira."Serikali ya kijiji imekuwa ikikusanya fedha na kufanya kazi za kutunza mazingira, sasa naona utaratibu huu mpya haueleweki," alisema Sandea.
Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Samunge, Michael Lengume alisema kijiji chao kwa sasa kinapokea idadi kubwa ya watu zaidi ya uwezo wake, hivyo kinapaswa kuwa na fedha za kuwezesha shughuli mbalimbali za kijamii.
"Tunafanya usafi, tunaboresha huduma ya maji, vyoo na masuala ya ulinzi na usalama hivyo, fedha hizi ni muhimu sana kwetu," alisema Lengume akipinga utaratibu mpya wa ukusanyaji unaosimamiwa na Halmashauri ya Ngorongoro. Hata hivyo, shughuli za usafi wa mazingira katika maeneo ya Kijiji cha Samunge unafanywa na wana mgambo waliopelekwa kijijini hapo na uongozi wa halmashauri wakitokea Vijiji vya Kisangiro, Yasimdito na maeneo mengine jirani, kutokana na vijana ambao ni wakazi wa eneo la Sonjo kukataa kushiriki katika kazi hiyo.
Kukataa kushiriki kwa vijana hao katika kazi ya usafi wa kijiji hicho, kunatokana na mila na desturi za Kabila la Wasonjo ambazo zinadai kwamba ni aibu kwa kijana hasa wa kiume kushiriki kazi za kufagia kufanya usafi hadharani.
Balozi apata kikombe
Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Burundi, Francis Mndolwa jana alipata kikombe cha Babu pamoja na baadhi ya wanafamilia wake.Balozi Mndolwa ambaye ni Brigedia Jenerali Mstaafu, mara baada ya kupata kikombe alipumzika kwa muda katika nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Elias Goroi na kuondoka baadaye.Nyumba ya DC Goroi imejengwa kijijini Samunge na inatazamana na eneo ambalo Mchungaji Mwasapila analitumia kugawa dawa.
Ndege zamiminika zaidi
Katika hatua nyingine, zaidi ya wafanyabiashara 49 wenye asili ya kiasia kutoka ndani na nje ya nchi juzi na jana walitua Samunge kwa ndege nne za kukodi kupata kikombe.Wafanyabiashara hao na familia zao, mara baada ya kutua uwanja mdogo wa Wasso, walipokewa na kupakiwa katika magari maalumu yaliyokuwa yameandaliwa na kupelekwa Samunge umbali wa takriban kilometa 70 na kupata kikombe.

CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment