ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 3, 2011

Baada ya kutanganzwa kuuliwa kwa Osama Ulinzi waongezeka maradufu NEw York City hasa sehemu ambayo milipuko ya 9 \ 11 ilitokea.

Siku tatu sasa toka kutangazwa kuuawa kwa kiongozi wa ugaidi Duniani Osama Ben Laden, Jiji la New York City ulinzi umeongezeka maradufu kila pande , hasa sehemu huska ya milipoko ya majengo marefu ya WTC. na ni kituo kukubwa na Train ya chini inayoelekea New Jersey ijulikanayo kwajina la PATH. Sehemu hiyo kama unavyoiona watu wanaendelea kuweka maua kama heshima ya kuwa kumbuka ndugu na jamaa, na vyombo vya habari kutoka kila pande wameweka kambi muda hapo hili mradi tu waweze kutoa habari  LIVE kutoka sehemu hii ambayo ujenzi wake unaendelea. Na pia wakimsubiri Mh Rais wa Marekani Barack Obama ambae anakuja siku ya alhamisi   kuongea na ndugu na jamaa  waliopoteza wapendwa wao. pia kuja kutoa shukrani kwa jeshi lake kwa kazi kubwa waliyoifanya na kufanikiwa kumwangamiza kiongozi huyo wa ugaidi duniani. Picha kwa hisani ya (NY Ebra wa NYC) alietembelea sehemu hiyo kuangalia hali inavyoendelea kwa sasa baada ya kutangazwa  kuuawa kwa Osama Ben Laden.
Ulinzi mkali ukiendelea New York City
Wakaazi wa mji huo wakiendelea kuweka maua Ground Zero
Waandishi wa vyombo mabali mbali vya habari ndani na nje ya Marekani wakiendelea kufunga mitambo yao kwa kuwatangazia wadau LIVE nini kinachoendelea Ground Zero

No comments: