WISDOM IS NOT MONOPOLY
Tusikubali
kuruhusu mioyo yetu ifadhaike.
Tusikubali
hata kama tunakwazwa kiasi gani.
Tusikubali
hata kama tunabomolewa kiasi gani.
Tusikubali
kwakuwa tunaporuhusu ndivyo tunazaa manun’guniko ambayo ni mwanzo wa kutenda
dhambi.
Kwamba,
badala yake
tuzikabidhi fadhaa zetu kwa Muumba huku tukiyakabili Matatizo yetu kwa kujua kuyafanya kuwa sehemu za changamoto zetu.
Lakini ni kweli,
hatuwezi kuwa chochote bila kufanya chochote.
Na
ndivyo basi,
tujifunze kugeuza Maisha kuwa Changamoto,
kwakuwa
Sisi
ni
Utatuzi wa Matatizo Yasiyoisha.
By Alex Kajumulo
UTANGULIZI
Mapenzi yakiisha,
je Maisha yanaendelea?
Sasa…
Lango la kwanza lilipofunguliwa ndivyo zaidi hofu ilinishika, kwani kuanzia hapo moyo uliripuka sana kiasi nilijikuta nikiacha kuzipiga hatua huku tayari miguu ikitetemeka; hatahivyo, sekunde kidogo zilivyopita nikaweza kupunguza hali hizo kupitia kuvuta pumzi kwa nguvu kidogo, na kisha kupumua kwa sana kiasi ndivyo walinzi walinitupia macho ya ghafla kwa namna nilihisi walisikia upumuaji huu.
Tena, nikajikaza kwa kupiga moyo konde na kuanza kutembea, lakini nikifanya taratibu zaidi kuliko ilivyokuwa awali huku tayari mwili mzima ukiendelea kutetemeka pamoja na kujitahidi usiweze kufanya kama sio kupunguza kasi…
Mara tena…
Ndio, lango lile likafungwa!
Lakini, hatahivyo, sikugeuka nyuma kwakuwa macho yote yaliganda hapo mbele ya lango la mwisho ambalo nalo lilifunguka mara nilipolifikia; na moja kwa moja, nikaingizwa ndani ya chumba kingine ambacho hisia zilieleza hicho kilikuwa.
Nywele zilisisimka pale mmoja wa walinzi waliokuwa wakiniongoza aliponiambia kwa sauti tulivu niketi katika kiti pekee kilichokuwepo katika chumba hiki ambacho kilikuwa katikati.
Nikajitupa...
Naam, niliketi huku msisimko ukiendelea kunitandika kwakuwa sasa hata akili zilisema ni hakika chumba hiki kilikuwa; na ni wakati huuhuu ndivyo sauti moja ilisemea kichwani huku ikiharisha usauti wa kejeli, ‘umekwisha!’
Mtu yule alikwenda nyuma ya kiti, akavuta mkanda mmoja, mara ukawa umenifunga kifuani; na hivyo, hata upande wa juu wa mikono ukawa umefungwa pia. Akavuta mkanda mwingine, nao ukanifunga kwa kupitia tumboni. Akafanya tena, hata mkanda mwingine zaidi nao ukawa umenifunga shingoni bila kuibana koo.
Nikatulia huku nikijikaza sana kupunguza hali za uhemaji ambazo hakika zilitaka kufyatuka…
Askari huyo akatoka huko nyuma yangu na kuja mbele; na nilipomtazama, aliinama chini ili kuyakwepesha macho yake. Halafu bila kunisemesha, akaanza kunifunga miguu kwa mikanda iliyokuwepo hapo. Na alipomaliza alitoa funguo mfukoni, akafungua zile pingu nilizofungwa miguuni, kisha ndipo akainuka kunifungua pingu za mikono...
“Tumeelezwa ungependelea aspen kuwa kitu chako cha mwisho, si ndivyo dada?” Mtu huyo alinisemesha mara baada ya kuwakabidhi wenzake pingu hizo huku mtu mwingine akinisogelea na akiwa amebeba kisahani kidogo ambacho niligundua kilikuwa kimebeba kipande cha sigara, ila sikuona kiberiti.
Nilitazama bila kujibu huku kwa kiasi nikihisi kuanza kuizoea hali kwani mitetemo ya mwili ilipungua sana ingawaje msisimko haukushuka.
Ndipo…mh, tena nikamuona yule mtu aliyenisemesha akiwa kakamata kiberiti cha gesi kilichokuwa tayari kinawaka maana macho yangu hayakufanikiwa kumuona akiiwasha.
Ndivyo sigara ile ikawashwa, kisha nikapewa.
Nami nikaichukua bila kutoa shukurani na kuipeleka mara moja mdomoni, kisha nilivuta pafu tatu za nguvu huku vidole vikiendelea kuishikilia; na taratibu, niliachia moshi ukitokea puani kwa namna nilikuwa nikiziitikia raha zake ingawaje ukweli ulikuwepo kuwa hizo hazikuweza kufua dafu katika kuniondoa ndani ya mawazo ya hofu yaliyokuwa yakikazana kuniumiza kihisia kiasi ndivyo niliichukulia (hii sigara) ilikuwa mithili ya minyororo iliyoongezwa kuhakikisha humo mawazoni siwezi kutoka kamwe, kwani nilithibitisha mawazo yalizidi sana kunivuruga huku jibu moja tu ndilo likikubalika kwamba hapa isingewezekana kuchoropoka!
Hatahivyo, sikuacha kuivuta sigara kwakuwa upande mwingine nilikiri ilijitahidi kunipatia ujasiri wa kusubiri, ujasiri wa kuunda hisia zisizoogopa!
Wale walinzi wengine waliniaga kwa pamoja na kisha wakatoka nje ya chumba hicho; na baadaye kidogo, yule mwingine naye akatoka na kuufunga mlango bila hata kuniaga, lakini alibakia katika kile chumba kingine, kile chumba cha awali.
Na hivyo, Gas-chamber ikabakia na mimi tu huku mwili ukielekea kurejea kutetemeka; lakini nashukuru kwa kiasi fulani ile sauti iliyosemea kichwani mwangu safari hii ilijitokeza tena kwa namna za kunipatia nguvu za kuufukuza uoga! Ndio, sauti hiyo ilisema, ‘mbona habari yako ni nafuu zaidi kuliko alivyotendwa Saddam kwa kamba lile!’
Kiasi mdomo ukafunguka…
Kiasi tabasamu likafanya…
Ee kiasi nilihisi kiasi…
Ee yote kwakuwa uraruzi wa hofu zangu ulibakia ukiitenda kazi yake…
“2” Nilibaki katika hali hiyo kwa dakika mbili tatu hivi, mara nikaanza kuwaona watu kadhaa wakija huku tazama zangu zikin’gamua kwamba kuta za vyumba vilifanyika kwa vioo tupu ambavyo ni lazima vilikuwa imara sana, maana vinginevyo...uh, ay sijui nisemeje!
Basi wale watu walipokuwa karibu sana, ndipo macho yakagongana na macho fulani na kufuatiwa na kuhisi kuchomwa moyoni na kitu chenye ncha kali lakini kikichoma kwa mpeleko wa raha; ndio, yalikuwa macho ya John Kusila! Na hata ikawa kwa mara ya kwanza tangu nikamatwe, niliweza kuhisi raha fulani ikinitambaa kiasi mwili mzima ukawa ukiondoshwa katika kutetemeka kwasababu za hofu hizi na kuanza kuchemka huku hali za ubaridibaridi zikipata kunikun’guta kiasi ndivyo nilisisimka hasa na hata kujikuta nikitamani nipigwe ngwala za raha!
Ewe msomaji, nadhani ‘hiki kitu’ ndicho nilistahiki nikipate, maana…mh, ee nilikosea kuchagua nipewe sigara! Lakini hatahivyo, nani angeruhusu nipatiwe kama ningesema nilihitaji?
Bado tazamo zetu zilikuwa zimeelekezana!
Kwamba, kila mmoja akimkodolea mwenzake kiasi punde kidogo hivi ndipo niliona...ah, Yaallah! Uh, asali wangu alikuwa akimwaga!
Ndio, akilia machozi!
Hata nika…uh, naam, nilitamani sana iwezekane ili nimfuate nimpanguse huku ndivyo nikiiumauma sigara kwani hisia kali zilianza kuninata huku ile ‘minyororo ya mawazoni’ kama vile ikiachiachia katika kuruhusu nichoropoke!
Ndivyo…
Mh, taratibu nikiwa vilevile natazamana na Kusila wangu nilianza kupotea mawazoni kwa kuhisi nikisafirishwa safari ya kurudi nyuma huku ndivyo nikizidi kuhisi mwili ulihitaji kupokea ujotojoto wa mwanaume niliyempenda kupindukia; ndio, hali hii hata ilifanya eti machungu yalitoweka huku kwa mbali nikihisi nikishikwashikwa, kwamba matiti yangu kama vile yalikuwa yakichezewa na mikono milaini niliyoifahamu sana! Au niseme hivi, ati ile mikono ya Kusila ilibinyabinya; ndio, hiyo ilifanya hadi mambo yaliharibika kulee ambapo wala siwezi kueleza zaidi ya kukutanabaishia kwamba yote hayo ilikuwa ni matokeo ya jibu lenye kiu za raha…
Bado sikuachiwa; ndio, hisia zilinisafirisha mbele zaidi hadi kuanza kuona kama vile sasa nilikuwa chumbani, ee eti sasa nilijiona tulikuwa chumbani pamoja na mwanaume tukiwa tumelala huku raha ikinipokea kwa toka zake za kuingiaingia…
Ee au niseme hivi: hapa sasa nilihisi mpeleko wa mkandamizaji akikandamiza kimkandamizo; yaani, huyo mkandamizaji alikuwa yuleyule handsome wangu John Kusila aliyebahatika kupewa kibali cha kunin’goa jino lisiloota tena kiasi hata hivi nilifanyika kuwa ni mwenye mwanya huu wenye uruhusu kwa yeyote mwenye kupeleka apeleke ilimradi aidha ridhaa yangu inakuwa imesema au vinginevyo ‘mbakaji’ anakuwa kalazimisha kwakuwa mwanya upo vilevile ukiwa wazi kwa uingiaji na kutoka!
Ndio, huyo mkandamizaji alikuwa mwanaume mweupe na mrefu kiasi huku akiwa na kifua kipana kilichojazwa kwa wastani na ‘majani laini, majani ya Aden’!
“3” Ni kwamba, huyo mkandamizaji au huyo John Kusila tulifahamiana kwa mara ya kwanza Kanisani ambapo sote tulikuwa wanakwaya. Kwanza, uhusiano wetu ulikuwa ni wa mwalimu na mwanafunzi wake waliokuwa na ukaribu wa kawaida; lakini taratibu uhusiano ulikuwa ukiimarika siku hata siku hadi hatimaye tulijikuta tukifikia mahala tukawa wapenzi ingawaje hivyo tulifanya kwa kupeana masharti tusubiriane hadi tutakapomaliza masomo ndipo uruhusu wa kufanya yaliyopaswa ufanyike.
Isitoshe, sote tulikuwa wanafunzi katika shule ya Shaabani Robert ambapo Kusila alikuwa kidato cha tano, mimi nikiwa kidato cha nne.
Ndio, ila uhusiano wetu wa kimapenzi ulianza kwa kuhakikisha tunaliweka pembeni tendo la ngono, kwani tulijipiga marufuku kujitumbukiza huko; tena hata wazazi wetu walifahamu kuwa sisi tulikuwa tukipendana kwa dhati huku wakitusisitiza tusithubutu kuutupa mgongo msimamo wetu...ndio, wazazi walituhasa tuendelee kuwa imara katika kuishi hivyo tulivyokuwa tumekubaliana hadi wakati muafaka utimie ndipo kila mmoja amtumbukize mwenzake katika uwanja ambao lazima mwanamke aondoke huku tayari utobozi umetendeka kwa maumivu yenye raha.
Basi, hapo kitandani nilipokuwa nikihisi nilikuwepo, ilikuwa ni kwasababu Kusila alidai alikuwa akiumwa, na eti hapo nilifika kumjulia hali! Na kwamba, nilipofika nilimkuta akiwa peke yake kwani wazazi wake na nduguze hawakuwapo; isipokuwa alikuwepo mtumishi wao wa ndani.
Tena hisia zilisema…
Ndio, hizo ziliendelea kusema eti Kusila alipoisikia sauti yangu, mara moja aliamka; na…eti zaidi alitenda kwa kunikumbatia!
Tena…
Oh, eti nami niliitikia kwa kuzidisha kukumbatiana huko kiasi kumbe shuka ilisogea pembeni hadi mara…kheh!
Mwanaume alibakia…ow! Mamaah!
Eh…nisemeje tena, maana hisia zilinieleza zaidi kuwa nikiwa katika hali ile eti ndivyo nilishtuka sana kiasi hata nilisitisha kuendelea kutuma yale majibu ya mahaba niliyokuwa nikimfanyia huku nikisisimka sana maana tayari macho yalikuwa yamekwishatazama hata kama niliyakwepesha haraka yasitize ukodozi; hatahivyo, nilijaribu kuzidhibiti hali zisizidi kunipeleka huko akili zilipokuwa hazitaki nipelekwe ingawaje ni kweli mwili ulitamani sana upelekwe hukohuko ili ikiwezekana…basi, ee liwalo na liwe!
Huku akili bado ikijaribu kuendelea kugoma na hivyo kuwa mpinzani wa tamaa za mwili (kama hisia zilivyosema), ndivyo nilijikuta nikigeuka mwili mzima ingawa bado nilikuwa ndani ya himaya za mikono yake ambayo licha ya kujilegeza lakini ilijua kunin’gan’gania ikinikumbatia huku halikadhalika akihakikisha haikuchoka kunitambaa…
Zaidi nilitenda katika kutaka kujikwanyua, lakini hatahivyo, niliishia kushindwa; isitoshe, hivyo nilifanya huku ‘hofu ya kuhitaji’ ikinijaa kiasi cha kuufanya usisimkaji wangu kuchanganyikana na mitetemo fulani, ingawaje bado ilikuwepo ile hofu nyingine iliyoletwa na tafsiri za akilini kwamba nilikuwa nachezea eneo la huruma za mamba!
“Mpenzi, kweli siumwi!” Kusila alisema huku akinipumulia sikioni huku akinivuta.
“Sasa mbona umeniita...?”
“Si vibaya kukuita wewe nikupendaye!” Alinijibu kwa kunikatiza huku bado akiendeleza mchezo wake wa kuyachezea matiti huku mara ulimi wake ukijipatia nafasi za kutambaa katika shingo yangu na kiasi ukiteremka kabla ya kupanda tena na kuendelea kutalii sehemu kubwa zaidi ya shingo ambayo kusema kweli ilikuwa ikipigika hasa kwa kunaswa na paruzaji zenye mitekenyo isiyoelezeka yenye raha zake.
‘Leo, sijui itakuwaje!’ Nilisema moyoni huku nikihemahema.
“Niachie dear! Ebu vaa bwana!”
Wala haikuonekana dalili kwamba alinisikiliza; na ndivyo kasi za uhemaji zilinitenda maradufu.
Lakini tena nilisema kwa kujitahidi kuukunja uso ambao hata hivyo badala yake ulirudi katika kutabasamu kabla sijamaliza usemi, “hivi mwenzangu hujioni? Mh, huoni…eh?”
“Babaa hujioni hukoje hapa?” Nilijitutumua tena huku ikizidi kubainika kwamba mwili ulizidi kusogezwa akili isipotaka; na isitoshe hata macho yalianza kulegea huku pia nikihisi ulegevu wa mwili ukisogea zaidi na zaidi...
Kidogo tena aliniachia huku bado nikitweta, kisha ndipo akasimama; lakini…mara tena, uh!
Naam, nilichapwa busu zito la shavu kiasi hapohapo mapigo ya moyo yakanienda kasi hata nikataka kusema neno, lakini mdomo ukawa mzito na hivyo kubakia umeachama kwasababu ndivyo nilihema sana!
Kidogo akaacha, lakini taratibu alisogeza kichwa huku ulegevu wa mikono yake ukifanyika mithili kama vile sasa alipanga kunitoa kifungoni ili pengine niwe huru...
Lakini wakati nikianza kuelekea kutaka kujichoropoa huku ulegevu wa mwili ndio ukiwa umesogea mbali sana, ndivyo nilishtukia kumbe nikigeuzwa mithili ya samaki kikaangoni; na ilivyokwenda zaidi ndivyo nilishtukia nikivutwa kiasi miili yetu iliposhikana ndivyo matiti yangu yalijibonyeza katika kifua chake ambapo nilipata ujotojoto wake huku yale ‘majani laini’ ndivyo yakinichomachoma…
Kisha, akapitisha…
Ndio, ulimi wa mwanaume hata ulipitiliza…
Ay? Jamani nisemeje, maana…ah, halafu, ikawa tena kama vile alikuwa akinisukutua mithili huo ulimi ulikuwa ni mswaki; na kiasi ndivyo nilizidi kulegea na nikiweweseka sana sana! Na muondoko haukuishia hapo, kwani mikono yake ilizidi kujipatia ruhusa kwa kunitomasa matitini huku wakati fulani ikihama kwa kujiteremsha kwenda chini zaidi na halafu ikiishia kwa kufanya mithili ikishtukashtuka kiasi mara tena hiyoo ikirejea huku juu…lakini…ah, halafu tena hiyo ikigeuza mwelekeo kwa kurejea kwenda huko chini kabla ya kutenda vilevile kwa kureja tena juu!
Mimi uh, mara nathibiti hivi; lakini mara tena…uh, ndio kidogo nateleza, kwamba, najikuta naachia tena...
Lakini huyoo…ah, ee eti tena nakaza uzi, kwamba majeshi yanazidisha uimara; yaani, nakuambia nilikuwa natwetatweta tu huku faidi za raha nikitamani ziongeze kasi katika kuupanda mlima wa mapenzi huku wakati huohuo hofu zangu zikilia kwa kunihabarisha sasa nilikuwa nikikaribisha ‘majuto mjukuu’!
“Mpenzi, wajua siumwi lolote...ila…ee ni kweli naugua kwakuwa imeshindikana nisiugue hivi ninavyougua hapa!”
“Sielewi unavyosema.” Nilijibu kwa kubwabwaja kwani bado nilikuwa nikitendewa ile ambayo sikuwahi kutendewa maishani!
“Kweli hujui, ila unafahamu maana wajionea!”
Nilimjibu kwa kuachia mguno wa kuuliza.
“Tiba ni wewe.” Alisema huku mdomo wake ukirejea katika kunipulizia hewa masikioni kiasi nilijikuta nikiwashwa sana huku nikihisi kulewalewa halikadhalika!
II
Mpekecho wa ghafla huko masikioni mwangu ulizifanya hisia hizi kuyeyuka huku tayari mwili ukiwa umechemshwa sana na nguvu za hisia hizi; lakini hatahivyo, wala haukupita muda mwingi huku nikihemahema kama kifaru aliyetoka kukimbiza ‘msosi uliochoropoka’, mara fahamu zilirejea huku kwa spidi kubwa sana nikibebwa na fahamu zangu kwamba bado tulikuwa tukiwa namna ileile kila mmoja akimtumbulia mwenzake kwa shauku!
Tena sauti ikapekecha masikioni...
Tena, ndivyo nikaacha kumtazama, na kuanza kugeuza shingo kidogo kuelekea huko sauti ilipokuwa imetokea huku halikadhalika nikielekeza tazamo langu hukohuko...
“2” Naam, ndipo nikabaini lile lango la mwanzo lilifunguliwa ili kumruhusu mtu mmoja kuingia…
Nikamkodolea sana mtu huyu ambaye sasa alikuwa chini ya upekuzi wa kiasi; na kulingana na muonekano wa namna alivyovalia ndivyo haikuwa shida kutambua alikuwa Mchungaji!
Baada ya kusachiwa, mtu huyu aliyeonekana bila wasiwasi kuwa mtu aliyekula chumvi kiasi aliruhusiwa kuniona; na hivyo lango la Gas-chamber likafunguliwa…
Ndivyo Mtumishi wa Bwana akaingia ndani…
Kisha tukaachwa wawili kwa kufungiwa…
“Bwana asifiwe.”
Badala ya kumjibu, nilivuta moshi mwingi na kisha nikauachia kidogokidogo ukitokea katika matundu yote ya pua huku mawazoni nikieleza sikuhitaji ujio wake kama ndivyo alidhani…
Bado alitabasamu na kisha akaketi katika kiti ambacho bila shaka kililetwa kwa ajili yake; kwamba, hakuonyesha masikitiko nilivyouitikia ujio wake kwa kumuanikia wazi dharau.
“Amani ya Bwana itufunike.” Aliniambia tena.
Nilibebetua mdomo na kisha ndipo sasa nilisema, lakini nikifanya kwa sauti ndogo, “hujui Mlango wa Bwana umefungwa kwakuwa muda umekwisha. Ndio, kwanza mhalifu kama mimi haiwezekani nifunguliwe hata kama muda ungekuwepo maana dhambi zangu ni msingi wa dhambi!”
Huyo alinikodolea kwa macho ya huruma.
“Halafu Babaa, haya siyaneni mimi, ila Andiko latamka waziwazi…mh, ndio, kila mtu atabeba msalaba wake!” Niliwahi kumueleza kwa namna za kuweka msisitizo zaidi, maana niliona Mzee huyu kweli alifika lakini bahati mbaya niliona alikuwa akipoteza bure muda wake; na hivyo, ndivyo niliona ilikuwa ni heri angeenda kuwahubiria watu wengine ambao muda bado uliruhusu katika kuupokea Wokovu wa Bwana kwani mimi tayari nilijipokea kuwa tayari niliishahukumiwa niende kuishi na Shetani.
“Mchungaji, huu ni msalaba ambao mimi mwenyewe nilijitwika...and i fully accept the consequences be it what kwani niliishi hivi!”
Lakini, mara…?
Mh, yaani ilikuwa kama niliyemchokonoa mchungaji huyu, kwani mara alianza kunihubiri na akifanya kwa hatua za taratibu taratibu kiasi kutamakia hata kweli nilijikuta nikianza kumsikiliza huku nikitafsiri haikuwa kwamba hakuwa akipoteza muda kama uchwara wa uelewa wangu kuhusu mambo ya kiroho ulivyokuwa ukinisemea!
Ndio, nilianza kumsikiliza kwa makini huku nikitii nilikuwa napelekwa kujiwasilisha mbele za Bwana nisivyotegemea! Pengine hivi nilikuwa nikivutika kwakuwa mahubiri yalifaulu hatua kwa hatua kuzinasa hisia na ufikiri wangu kiasi nilitulia kimya mithili ya maji ndani ya mtungi; tena hivyo ilitendeka kwa namna hata Kusila wangu hakutazamwa tena mithili alisahauliwa!
Hata ndivyo kutamakia nilifika katika kulia kwa machungu kiasi Mchungaji alijikuta akianza kunibembeleza huku akizidi kunilisha Chakula ya Roho…
“Mwanangu nakuomba usali moyoni mwako kwa sababu Sala si kwa ajili ya Bwana, ni kwa ajili yako mwenyewe. Na isitoshe, ni kwa kupitia Imani yako ndivyo Sala na Matendo yako vyote huchangia kukubadilisha kwakuwa yakupasa kutembea kikamilifu na Bwana!”
“Ukimpokea sasa tayari, umekamilika. Na ndivyo ataishi ndani mwako akikutendea makuu usiyoweza kufikiri…ebu mpatie nafasi akujibu!”
“Mchungaji, mimi nimekufa tayari…atanijibuje zaidi ya kunihukumu kama alivyoahidi kuwaadhibu wakosefu?” Nilimueleza Mchungaji huku bado nikilia kwani ni hakika maneno yake yalikuwa yakiingia barabara akilini.
“Bwana ni mwema, Bwana ni mpole…naomba fanya toba akusamehe!” Mchungaji alisimama kusema kwa kutulia sekunde chache kama vile kichwani mwake kulikuwepo na ufikiri fulani, kisha aliendelea kusema lakini safari hii akifanya kwa taratibu sana, “ahm…wajua, ah, Bwana ananionyesha…mh, haupo peke yako, kwani naziona ishara kuna wengine wapo humu wakiwa ni uchafu unaotakiwa kukazana kuufukuza ili Heri za Bwana zifanye makazi ndani yako kabla ile saa haijafika ambayo wajua haipo mbali.”
“Kweli Mchungaji?” Ndio, nilipayuka; tena hivyo nilifanya bila kujua kwanini nilifanya!
“Ukimtumaini Yeye aliye zaidi ya Nabii, Yeye aliye Mkuu zaidi ya Wakuu wote, utashinda. Kwani Kwake kila jambo huwezekana kwa yeye ampendaye Bwana na kumtumaini! Tafashali, mwanangu anza sasa, kwakuwa hujachelewa!”
Hapo ndipo hasa nilifanya, kwanza kwa kuitupa sigara, na kisha niliungama kwa kutubu hadi kujikuta nikiishia kwa kuusema ubeti mmoja ambao ni huyuhuyu John Kusila aliwahi kunifundisha bila kueleza wapi aliutoa.
Ndivyo niliishia nikisali hivi kwa unyenyekevu kwa kujisalimisha kidhalili mbele za Muumba -
Ee Mungu,
nifanye Chombo cha Amani yako;
palipo na Chuki nipande Mbegu ya Upendo,
palipo na Mateso nionyeshe Huruma,
palipo na Giza nionyeshe Mwangaza,
palipo na Mashaka unipe Imani,
palipo na Unyonge unipe Tumaini,
palipo na Huzuni unipe furaha...
Ee Mungu,
Mbele zako sihitajiki kuliweka Tumaini Hai;
bali kupitia WEWE Tumaini ndilo laniweka Hai
kwakuwa napaswa kuishi ndani yake…
Ee Mungu, na hapa nayenyekea kwa kuishi hivyo…
Na baada ya nusu saa hivi, ndipo Mchungaji aliniaga huku akisema kwa kuachia sauti ndogo lakini iliyoongezea kuzionyesha hali zake za kunihurumia, “Amani ya Bwana iendelee kumulika mapito yako hata Mahala pema ukalale kwa Upendo wa Bwana!”
Nikaitikia kwa unyenyekevu, kisha Mchungaji akafunguliwa mlango, akaondoka huku nikimuona haishi kugeuka nyuma na kunitazama sana kwa macho yaleyale yaliyojaa huruma…
Na ndivyo nikaachwa tena mimi na mwili wangu uliokuwa sasa ukitema jasho kwasababu ile hofu ilirudi kwa kasi huku nikinyon’gonyea; lakini hatahivyo, sauti fulani ikawa ikisemea huku mawazoni mwangu kama sehemu ya mimi iliyokuwa ikipigana katika kunijenga kitumaini…ndio, hiyo ilisema kwa kurudiarudia maneno, ‘Mbele za Mungu hauhitaji kuliweka Tumaini Hai kwakuwa hilo latoka kwa Bwana kukuweka wewe hai, hivyo, jihifadhi ndani ya Tumaini hili…
Mbele ya chumba hiki kulikuwa na saa. Nikawa nikiitazama jinsi mishale yake ilivyokuwa ikitembea; na kwakweli niliona kama ilikuwa ikienda kwa haraka sana kuliko kawaida, kwani jinsi ilivyokuwa ikienda ndivyo nami nilizidi kunyon’gonyea maana tayari nilianza kuhisi roho kulazimishwa kunikimbia…
III
Nini kilipeleka hasa hata hivi nilifikishwa?
Ndugu msomaji, mkasa huu kunikuta ni habari ndefu, habari ambayo iliyabadilisha maisha yangu kuwa ya kifukara huku kitabia nikiwa mchafu kabla ya kurejeshwa tena katika maisha mazuri kama nilivyokuwa tangu kuzaliwa kwangu; lakini kurejeshwa huko kulikuwa kwa muda mfupi sana, maana nilivamiwa tena kiasi huku nilijifikisha!
Kweli, hivi nikifikiri huumia sana kwani hakuna zaidi tena; ndio, hakuna zaidi ya huku kusubiri kunakotisha sana! Hatahivyo, yote namuachia Mungu, maana yeye ndiye anayejua nini nastahiki dhidi ya niliyofanya...ah, ingawaje huyu baba, ah? Yaani, nimehukumiwa adhabu ya kifo kwa sababu…?
“2” Nilishtushwa kwa sauti nzito; na ndivyo nikajikuta nikitolewa ghafla ndani ya kumbukumbu hizi huku mguno wa kuweweseka ukinitoka!
“Dada, wakati wako wa kusema neno la mwisho.” Nilisemeshwa tena; msemaji alikuwa askari mmoja aliyekuwa pandikizi la mtu akiwa amevaa fulana na kaptula. Huyo aliingia humu muda mrefu kidogo ambapo sikuwa nimeshtukia jinsi alivyoingia kutokana na kubanwa kule na mawazo yangu. Si unajua mambo ya mawazo na huu uoga wa kuuawa!...we tazama tu na usiombee yakufike, maana...ah, sina la kusema!
Na mara akaitwa; ndio, John Kusila aliitwa ambapo kabla ya kuanza kuingizwa ndani, niliona jinsi walivyomsachi. Na aliporuhusiwa, akaingizwa kile chumba cha mwanzo; na huko sauti zote nilizisikia.
“Mnaweza kuzungumza.”
Nikajiuma meno nikijitahidi kutaka kusema...
Hatimaye niliweza ingawa moyoni nilibakia nikijiona niliyemkosefu mkubwa kiasi hata machozi yalianza tena kunichuruzika, “Mpenzi, sina zaidi la kunena; isipokuwa nimekuita hapa ili unitamkie kama kweli umenisamehe.”
Tuliiweka mikono yetu katika mkao ambao kama tungekuwa ndani ya chumba kimoja basi ingekutana sawia, lakini hivyo haikuwezekana kwani tuliachanishwa na ukuta mzito wa kioo!
Hatahivyo, hisia zangu zilitengeneza hali mithili niliweza kugusana na hali zake za ujotojoto!
“Nafahamu sana. Usijali kwani yote yaliyopita ni mitikisiko ya dunia ambayo hata mimi ingeweza kunivaa. Nenda ukitambua nimekusamehe. Ndio, nimekusamehe kwakuwa mshamrashamra za dunia zilikuzidia ambapo kwa bahati mbaya sana ulijisahau au hukuweza kushambulia kulinda kile ambacho mimi mwenzako nilisimama imara na daima kukilinda! You’re forgiven my love and hope God will do the same!”
“Ahsante! Ahsante sana!” Nilijibu, kisha nikaachama kuikenua furaha.
Huku nikizidi kusahaulishwa machungu, zaidi alinitendea kwa kuusogeza mdomo wake hadi…
Ndio, aliugusisha ukutani!
Nikaelewa!
Nami nilifanya pia; na hivyo tulifikia katika kuhisi kweli tulikuwa tukifyonzana huku kila mmoja akisikiliza jinsi mapigo ya moyo wa mwenzake yalivyokuwa yakiachia sauti zake!
Muda kidogo, niliacha kuulamba ukuta huo, na kisha nilisema, “mdogo wangu atakupatia zawadi.”
“Zawadi?” Alishtuka.
“Kwamba nashukuru umenisamehe.”
“Kama unalipa, umetenda kosa jingine.” Kusila alijibu na tena aliendelea, “msamaha wangu si kwa ajili ya kulipwa...unasikia my love?”
“Oh, hapana darling! Naomba uchukue kwa sababu mimi nikupendaye nimetoa kwa ridhaa na furaha zangu hata kama usingenisamehe!”
Kabla hajanijibu, nilisema, “halafu, shiriki kutunza mwanangu.”
“Huhitaji kusema hili.”
Macho ndiyo yalijibu.
Muda ulipotimu tulianza kuagana…
“Nasisitiza...saidia kumtunza mwanangu ambaye nilizaa na…oh, masikini miye!.” Nilishindwa kumalizia kwani hapohapo matone kadhaa ya machozi yalikaribishwa tena, na ikabidi niipatie mikono kazi ya kuyafuta, ingawaje, hatahivyo, pamoja na yote hayo bado kwa ndani nilikuwa mwingi wa furaha kwani uoga ulikuwa haujarejea. Humu niliona kama palikuwa sehemu ya kawaida.
Kusila alitingisha kichwa huku akianza kuondoka ndani ya chumba hicho kwani askari aliyekuwemo humo alianza kumsumbua kuwa muda ulikuwa umekatika.
“3” Sauti ya askari ilinieleza, “Dada, ebu weka mikono vizuri.”
Nilifanya kama alivyoelekeza askari huyu aliyekuwa pandikizi la kiumbe huku utazamaji wake ukiwa wenye tafsiri ya mtu asiyejali. Naam, tena nikafungwa hata mikono yote; nikawaona watazamaji wakinitazama kwa macho ya huzuni.
Ee saa ilikuwa imetimu!
Pia nilimuona Charlie, kidogo nilitabasamu!
Pia nikawaona wale waliokuwa malaya wenzangu wakiwa pamoja na wifi yangu, yaani mke wa Gushuradhi hata nikataka kuwapungia mkono lakini nikashindwa, maana nikakumbuka kuwa mikono ilikuwa tayari imefungwa!
“Dada kwaeri.” Lile baba likanitibua tena kwa kunishtua. Likaendelea kusema, “Gesi ikianza kutoka ivute kwa nguvu zaidi; na hivyo ndivyo utafariki vizuri, na kwa haraka sana. Vinginevyo, utakufa kwa kuteseka sana!”
Askari huyo akafungua mlango na kutoka na kisha tena akanifungia na kuniacha peke yangu. Hapo ndipo kijasho kikaanza kunitoka, kwani ule ujasiri niliokuwa nao mara ulitoweka, yaani, ulikuwa sawa na kusema, ‘ulinipiga chenga ya mwili na kuniacha kwenye mataa!’
Ndivyo, nilitetemeka sana haijapata kutokea maishani; kwamba kila kitu kilitetemeka kuanzia mwili wote, moyo wote, na roho ambayo nilihisi haikuwa imependa kuyaacha maumbile!
Mara nikahisi chumba kuanza kubadilika harufu, na mara nguo zangu zilianza kulowanishwa kwa majimaji nisiyoelewa wapi yalitokea; ndivyo nikajaribu kupinga nikibana pumzi, nikajaribu sana, nikafanya sana…
MPENDWA MSOMAJI, ILI KUJUA YOTE JITAYARISHE KUKISOMA KITABU KIZIMA KWANI KINATOKA MWEZI WA SABA HUKU VINGINE VIKIFUATIA…
1 comment:
Kupitis utunzi mkuu na wazo kuu kutoka kwa Alex Kajumulo, kitabu hiki kinaeleza namna madhara ambayo wanaume (mafataki)wanaodanganya mabinti wanafunzi katika kuwaingiza katika maisha ya ngono yanavyoweza kuharibu mtiririko wa maisha kwa wanaozaliwa katika uovu huu kiasi cha kushindwa kuhimili ipasavyo vishindo vya fadhaa wanavyovipata maishani mwao!
lakini pia kitabu hiki kinaeleza matokeo ya kufanya uamuzi usiokuwa sahihi unavyoweza kuzaa madhara zaidi au fadhaa zaidi!
usikose kukisoma kitabu hiki chenye mafunzo mengi ambayo zipo sehemu ambazo Mtunzi Mkuu Mr Alex Kajumulo alipitia katika kasi yake kimaisha kama anavyoiita mwenyewe 'amazing race' ambayo pia anaitayarisha kuwa kitabu na kufanywa filamu katika kuwathibitishia vijana kwamba wakiwa na dhamira thabiti na uthubutu wa vitendo thabiti ndivyo wanaweza kufikia malengo wanayoyataka wayapate maishani mwao.
Usikose...july kinatia timu!
Post a Comment