*NI MHITIMU MWENYE SHAHADA TATU IKIWEMO YA URUBANI
*ANAMILIKI KAMPUNI YA TANJET INAYOSHUGHULIKA NA NDEGE BINAFSI
Mkurugenzi wa TanJet Hangar Susan Mashibe akilongo na MO BLOG.
MO BLOG : Kama MO BLOG na wadau wetu tungependa kufahamu Susan Mashibe ni nani hasa….?
MASHIBE : Mimi ni mtu complex sana. Lakini labda nianze kwa kuelezea my educational background. Mimi nimesomea uhandisi wa ndege, urubani wa ndege na vile vile management ya ndege. Kwa sasa hivi mimi ni mjasiriamali katika hii sekta ya usafiri wa anga.
MO BLOG : Susan tuambie umeanzia wapi hadi kufikia hapa ulipo..? Kwa maana ya kwamba ilikuwa ni mipango yako kusomea masomo hayo au hali ya maisha imekufanya ukajikuta katika fani hii..?
MASHIBE : Nilikuwa na nia ya kutaka kurusha ndege tangu nikiwa na miaka minne.Mapenzi yangu kwa ndege yalianza wakati wazazi wangu na mimi tulikuwa tunaishi Kigoma. Kipindi Fulani wazazi wakawa wanasafiri kutoka Kigoma kuja Dar es Salaam. Wakaondoka na wadogo zangu wawili, mimi wakaniacha na bibi ambaye alikuwa amekuja kuniangalia. Ndege ilipokuwa inaondoka roho iliniuma sana, nikasema ningekuwa naweza kurusha ile ndege wasingeniacha. Kwa hiyo nikapata hamu sana ya kurusha ndege ili siku nyingine wasiniache. Kipindi hicho niko na miaka minne lakini sikuwa yule mtoto wa kulia lia kwamba nimeachwa na mama, mimi nilikuwa mtoto wa kufikiria sana, huwa nafikiria, nasema nataka kitu fulani, kweli siogopi nakiendea na nafanikiwa.
MO BLOG : Kutokana sasa na nia uliokuwa nayo. Tufahamishe ulianzia wapi kielimu mpaka kufikia kutimiza malengo yako ya urubani wa ndege..?
MASHIBE : Nilipomaliza form four nilichaguliwa kwenda chuo cha ualimu, lakini mapenzi yangu yalikuwa kwenye ndege. Yani kulikuwa hakuna kitu kingine nilikuwa napenda nifanye zaidi ya ndege. Wakati huo tayari dada yangu alikuwa yuko Marekani, kwa hiyo nikapata nafasi ya kwenda Marekani kusoma. Maana baada ya kumaliza form four mimi sikusoma form five walasix. Nilimaliza Pamba Sekondari pale Mwanza baada ya hapo nikaenda Marekani. Na nilipofika kule nilikuwa siwezi hata kuongea kiingereza na ili uweze kurusha ndege ni lazima u-communicate na control tower kwa kiingereza. Hivyo mwalimu wangu akanishauri kabla hawajaniruhusu kwenda solo (Solo ni kuruhusiwa kurusha ndege peke yako bila mwalimu, ukiwa na mwalimu inaitwa duo) nijifunze kwanza kujieleza na kuongea. Nikaona hiyo itanichukua muda. Nikasema wakati najifunza kuongea pia nataka nijifunze kila kitu kuhusu ndege. Na kulikuwa na chuo cha uhandisi wa ndege karibia na kule nilikokuwa naishi. Nikaenda nikajiandikisha. Nikasema nataka kusoma uhandisi wa ndege, kwa sababu nilijua mimi nilikuwa napenda sana masomo kama Physics na hesabu hivyo nikajua darasani theory haitanisumbua sana. Kwa sababu hesabu ni numbers hazina lugha na kama ni laws za physics ni laws tu. Nikaju pia nitachukua madarasa ya kuongea English. Nikajikuta mpaka nakuwa fluent in English tayari nimeshamaliza masomo yote ya uhandisi na nikafanya mtihani wa taifa wa uhandisi wa Marekani wa Civil Aviation yao inayoitwa FAA. Nikapass na nikajikuta nimekuwa mhandisi japo haukuwa mpango wangu kuwa mhandisi. Sasa kutokana na gharama za mafunzo ya ndege kuwa kubwa ilibidi nifanyekazi kama mhandisi ili niweze kujilipia mwenyewe mafunzo hayo. Nikawa nafanyakazi usiku ya kutengeneza ndege mchana na kwenda kurusha. Ili uweze kukaa kule inabidi kujiandikisha kuwa mwanafunzifulltime hivyo nikalazimika kujiandikisha na nikajikuta nasoma Aviation Management. Kwa hiyo mazingira kwa ujumla yakasababisha mpaka nilivyokuja kumaliza vyote nimekuwa Mhandisi, Rubani na Meneja wa Mambo ya Ndege.
Susan Mashibe akifanya mahojiano na Lemmy Hipolite wa MO BLOG.
MO BLOG : Imekuchukua muda gani/miaka mingapi mpaka kumaliza vyote hivyo..?
MASHIBE : Ahhh…!! Imechukua muda mrefu maana nimekwenda Marekani mwaka 93. Uhandisi, Urubani na Management nimechukua kama miaka 9 na hizo ni Degree Tatu tofauti. Wakati huo gharama za kurusha ndege ilikuwa ni kama dola 90 ($90) kwa saa hivyo nilikuwa narusha kwa saa 2 kwa wiki kutokana na uwezo wa kifedha, kwa sababu nilikuwa natengeneza kama $ 12 tu kwa saa na natakiwa kulipia kurusha ndege, manejiment, kodi, gari, mafuta na mahitaji mengine hivyo nikalazimika kufanya kazi saaana. Nilipata leseni yangu ya kwanza mwaka 2000 na ya pili mwaka 2001 na ya tatu mwaka 2002.
MO BLOG : Ulipomaliza masomo na kuhitimu ulianza kufanya kazi Marekani moja kwa moja? Na ilikuaje ukarejea nyumbani Tanzania..?
MASHIBE : Kama nilivyosema mwanzo nilipojikuta nimekuwa mhandisi nililazimika kufanya kazi kama mhandisi ili nipate fedha za kulipia masomo niliyokusudia ya urubani. Na lengo langu nilitaka nikafanye kazi ya kurusha ndege katika mashirika makubwa kama Delta, kwa sababu nilitaka kurusha ndege aina ya Boeing 777. Sasa Napata leseni yangu mwaka 2001 wakati namalizia masomo nadhani kila mtu anakumbuka kilichotokea ile September 11 hali iliyopelekea industry ya ndege kuvurugika. Hata hiyo Delta yenyewe niliyotaka kwenda ililazimika kupunguza marubani hivyo nikagundua siwezi kupata kazi ndipo nikaanza kufikiria kurudi nyumbani.
Ilinichukua miaka miwili kutafuta kazi nyumbani na hakuna mtu aliyekuwa tayari kuniajiri. Lakini mwaka 2003 nikaamua kujiajiri mwenyewe hivyo I set my mind kuwa I will make it happen in Tanzania na hii yote ni kwa sababu ya mapenzi ya kazi hiyo. Nilikuwa naweza kubadili fani labda niingie katika media au nikabakia Marekani lakini nikasema hapana nakwenda Tanzania na nitafanya vitu vyangu.
2003 nikaanzisha kaofisi kangu ambapo mpaka leo kako pale uwanja wa ndege wa Dar. Nikaenda kuomba kupata hangar yaani eneo kubwa ambalo tunaweza kuweka hata ndege ndani, nikawaeleza what I want to do, wakaniambia kwanza sisi hata hatuelewi unaongea kitu gani.
Kwa kifupi mwanzo ulikuwa mgumu kwa sababu ile sector ambayo mimi nilikuwa nime specializeya ndege binafsi huku ilikuwa haipo. Watu walidhani mimi nikichaa, wakaniambia kama unataka biashara ya aina hiyo nenda Nairobi.
Kutokana na foleni za hapa mjini siku moja Dada Susan Mashibe aliamua kupaki Prado yake ofisini na kukodi Bajaj mpaka mjini ili aweza kuwahi mkutano.
MO BLOG : Wewe nini kilikupa msukumo wa kujiamini kuanzisha biashara ya aina hiyo hapa haswa baada ya kukatishwa tamaa na watu wa sekta yako.
MASHIBE : Kwanza nilishapiga hesabu mafuta ya ndege hapa Dar yalikuwa ni cheaper kuliko Mombasa na Nairobi mwaka huo wa 2003. Hivyo nikajua ukimwambia mtu njoo weka mafuta hapa atakuja na ukiweka zile huduma zako vizuri ukizingatia wateja ni watu executive.
Tofauti na huduma hiyo kwa ndege binafsi sisi ndio tulioanzisha system ya credit card zaAviation kwa Afrika Mashariki japo ilikuwa usumbufu sana mwanzoni.
MO BLOG : Sasa Bi. Susan Mnafanyaje ili kuwapata hawa wateja wanaotumia ndege binafsi maana ni watu maarufu na wenye fedha zao..?
MASHIBE : Kwa sasa unajua tunajulikana kutokana na huduma zetu tunavyotoa na jinsi tunajali muda wa mteja. Labda nikukumbushe tulipokua tukianza Julai 2003 tulipata ndege moja tu bahati nzuri ndege yenyewe ilikuwa ya JACOB ZUMA tukaihudumia vizuri hadi mwenyewe akafurahi jina likaanza kukua. Ikaja wakati wa mkutano wa SADC enzi za Mkapa na nilijieleza wale mapilot wa marais wakaamua kunijaribu kwa sababu nilikuwa naonekana kadogo, alafu hajawahi kusikia huduma zetu zikitolewa Tanzania. Walipata huduma nzuri katika ndege zao zote kama 12 hivi na hadi leo ni marafiki na kila wanakokwenda wanatangaza kwa wenzao wapite Tanzania watamkuta Susan watapata huduma nzuri.
Susan Mashibe On Google bus during March YGL Bay area Summit.
MO BLOG : Changamoto zipi unazokutana nazo katika utekelezaji wako wa majukumu ya kazi ya kila siku kama mwanamke..?
MASHIBE :Kwa kweli sijakutuna na changamoto katika utekelezaji kama mwanamke. Nadhani hii ni sabubu ya confidence na mie ni mpiganaji wa haki zangu mzuri sana. Labda niseme nakutana na changamoto kama mjasiriamali moja ya changamoto ni kuwa mwanzo tuliamua wafanyakazi wote wa kampuni hii wawe watanzania ili tuweze kutengeneza nafasi za kazi kwa watanzania wenzetu. Lakini vijana wengi wanashindwa kuendana na utamaduni wetu wa utendaji kazi na kuendana na mahitaji ya kikazi wanakuwa very slow. Hata hivyo naweza kusema staff nilionao wameimprove wanaweza kuendesha hizi shughuli bila hata mimi kuwepo. Hii ni succession plan.
Changamoto nyingine ni katika kudeal na authority mbali mbali. Kwa mfano unajua sisi tunakusanya mapato mengi sana na tunalipa serikali, lakini serikali bado iko nyuma sana katikapayment method bado wanapenda sana malipo ya cash. Fikiria unapata taarifa saa moja jioni kwamba ndege tatu saa nane usiku na itakaa kwa nusu saa, sasa saa hizo huwezi kwenda benki kuchukua hela ya kulipia mafuta na pia sio salama. Sasa wanao tuuzia mafuta saa nane usiku wanataka cash na wanasema hiyo ndege haiondoki mpaka ilipiwe. Hivyo ni usumbufu kwa ndege zetu maana unavuruga utaratibu wote wa safari. Inabidi serikali iwe na mfumo wa electronic payment. Huu mfumo utasaidia wadau wote na kuwezesha wadau to maximize mapato yao na kuboresha huduma kwa wateja.
Nyingine ni miundo mbinu, unapigiwa simu lakini huwezi kufika ulipoitwa au kazini kwa wakati muafaka kutokana na miundo mbinu kwa mfano barabara nadhani hili kila mtu analijua ila kubwa zaidi ni mgao wa umeme. Huu umeathiri sana sekta hii na kupunguza uzalishaji wetu.
Susan Mashibe akiendelea kuji express kwa MO BLOG.
MO BLOG : Unauzungumziaje usafiri wa anga kwa ujumla kwa hapa Tanzania pengine na duniani kwa ujumla.
MASHIBE : Yaani kusema ukweli tuko nyuma saana nchni kwenye hii industry, mfano Air Tanzania. Inasikitisha kuona kwa nini inashindwa kuperform wakati market ipo? Kwa sababu ni ndege nyingi za kutoka nje ndio zinazokuja ku- service market ya hapa kwetu. Ningependa wizara, serikali na mamlaka mbali mbali ziweze kutusaidia sisi wadau wa usafiri wa anga ili tuimarishe hii sekta kwa sababu tayari tunataaluma. Kwa mfano ukizungumza na wadau wote malalamiko yao yanafanana kwamba serikali haitupi uhuru. Na nashauri kwenye vile vitengo husika waweke watu ambao ni fani yao ili kurahisisha utendaji, kuliko unamkuta mtu halafu inabidi tena uanze kujieleza na kumfundisha ndipo akusaidie.
Wenzetu Kenya na Uganda wanakwenda kwa kasi, kwa mfano angalia Rwanda walikuwa na ndege moja tu tena DASH 80 lakini sasa wana JETS nyingi tu kwa sababu ya ushirikiano kati ya serikali na wadau. Ila naisifu saana Precision Air wamejitahidi wamefanya vizuri sana.
Hii ni moja ya kazi Susan Mashibe anayopendelea kuifanya Ndege zinapowasili na kuzihudumia yeye mwenyewe mbali na kuwa na wasaidizi.
MO BLOG : Nini ushauri wako, hatua zipi za makusudi zichukuliwe..?
MASHIBE : Ninachoweza kusema ni kuwa serikali iangilie namna gani inaweza kuingia na kulikamata soko la anga ikianzia na hapa nyumbani. Mfano kutoka Tanzania kwenda Tunisia ni lazima uende mpaka Ulaya kwanza ndio upate ndege ya kurudi Afrika ikuache tunisia hilo ni soko au kutoka Dar hadi Lubumbashi unatumisia siku nzima. Na wafanyabiashara wa Lubumbashi wanatumia bandari ya Dar. Usafiri was anga utasaidia uchumi kukua.
Susan Mashibe akiwa ndani ya TANJET FALCON 900 JET hii ni moja ya ndege itakayokuwa ikimilikiwa na kampuni hiyo.
MO BLLOG:Nini matarajio yako ya baadae?
MASHIBE : Sasa hivi tunaanzisha huduma ya matengenezo ya ndege yenye hadhi ya kimataifa. Pia tutaanza kutoa mafunzo ya urubani hivi karibuni na mafunzo ya uhandisi wa ndege baadae kidogo. Kwenye mambo ya jamii, mimi binafsi napenda sana kuwasaidia watoto wa kike walio shule za sekondari kufanya vema kwenye masomo ya hesabu na sayansi.
MASHIBE: Nawapenda sana watu waliojitoa kufanya mambo makubwa haswa vijana waliloliletea taifa hili maendeleo nikianza na Mh. Mohammed Dewji Mbunge, sikutegemea kama yeye ni kichwa cha MeTL na MO BLOG naomba watanzania waige mfano wake, na vijana alinao katika blog yake naomba Mungu awape uwezo…. Nawapenda sana…..BIG UP GUYS ….
Operation Manager wa MO BLOG Zainul Mzige katika picha ya kumbukumbu na Susan Mashibe.








No comments:
Post a Comment