- Aahidi Donge Nono Iwapo Itashinda
Na.Mwandishi wetu.
Mbunge Wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji Ameitakia Kila La Kheri Timu Ya Simba Katika Mchezo Wake Wa Kuwania Kufuzu Kwa Hatua Ya Makundi Katika Michuano Ya Klabu Bingwa Afrika Dhidi Ya Wydad Casablanca Ya Morocco.
Mh. Mo Amewaambia Simba Kuwa Yuko Pamoja Nao Katika Dua Akiwaombea Mafanikio Ili Waweze Kuvuka Kizingiti Kilichopo Mbele Yao Na Kuwapa Watanzania Furaha Kwa Kushinda Katika Mchezo Huo Utakaochezwa Juni 28 Mwaka Huu Mjini Cairo.
Amesema Kitendo Cha Rufaa Yao Kukubaliwa Huku Timu Ya Tp Mazembe Ikiondolewa Na Simba Kuendelea Ni Ishara Ya Nyota Njema, Hivyo Wasipoteze Nyota Hiyo Ambayo Tayari Imeshaanza Kung’aa Na Badala Yake Waing’arishe Zaidi Kwa Kuwaadhibu Wamorocco Hao.
Mo Amewataka Wachezaji Wa Simba Kuwa Na Ujasiri Na Kujiamini, Na Kuwataka Wakumbuke Kile Timu Ya Simba Ilichokifanya Katika Michuano Kama Hiyo Mwaka 2003 Kwa Kuwatoa Timu Ya Zamalek, Basi Warudie Kitendo Hicho Hicho Ili Historia Ya Simba Ijirudie Na Kuweka Heshima Katika Medani Ya Soka Tanzania Na Afrika Kwa Ujumla.
Aidha Ametaka Watanzania Wote Tuondoe Tofauti Za Usimba Na Uyanga Na Tushirikiane Pamoja Katika Kuiombea Simba Dua Ili Ishinde, Kwa Kuwa Ushindi Wa Simba Ni Wa Watanzania Wote Na Sio Wa Wana Msimbazi Peke Yao.

No comments:
Post a Comment