New England umoja inawakaribisha Wanajumuia wote, ndugu , jamaa na marafiki kuumgana nasi katika "fundraiser "ya aina yake kutunisha mfuko wa kuadhimisha miaka 10 ya Jumuia yetu kwenda Mohegan Sun casino, siku ya Jumamosi tarehe 28 Mwezi huu, kuanzia saa 4 Asubuhi, hadi saa 12 jioni.
Gharama za kila msafiri ni dola $35.00. Ada hiyo inakupatia "meal coupon" ya dola $15.00, ambayo inatosha kabisa kwa "buffet style dinner",na coupon ya dola $15 itakayokuwezesha kucheza tombola kwa wale watakao kwenda kucheza tombola . Ukiangalia gharama halisi ni Dola $5 tu!!. tafadhali jumuika nasi na usikose nafasi hii ya pekee na ya aina yake!. Let’s go and have FUN!!
Kwa wale wanaotaka kujiunga kwenda wawasiliane na
Maria Sombe 413-364-8146 au Hamadi Mkambavange. 413-221-2935
Basi litaondokea Springfield Saa 4 KAMILI! (10:AM Sharp) na litaondoka Mohegan Sun casino Saa 12 jioni (6:PM Sharp).Tunawaomba wote mjitokeze kwenda kwenye safari hii ili tufanikishe "fundraising" hii.Wajuulishe Marafiki zenu kazini, Clients wetu, ndugu ,jamaa na tuwape habari na kuwahamasisha ili tulifanikishe lengo letu. Ni njia rahisi ya kuchangia mfuko wetu wote tukiwa kitu kimoja. Mtu mmoja hawezi kulifanikisha hili peke yake!. Mpaka sasa hivi tumeshapata watu 16 ambao wako tayari kwenda. Tunahitaji watu 47 au zaidi ikujaza basi, li tupate faida ya dola $1000.00, baada ya kutoa gharama zote!!. We can make it happen!!!!.
New England umoja inawashukuru wale wote watakaojitokeza na kwenda pamoja nasi, au wale wote watakaoleta watu wa kwenda.
“YOU NEVER KNOW, IT COULD BE YOUR LUCKY DAY TO-BECOME A MILLIONAIRE!!!” Let's get ready to have some Fun!!!!!!
Karibuni sana wote.
No comments:
Post a Comment