ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 27, 2011

Kitanda kinahitaji busara, siyo upole wala mapepe-GPL

TUMSHUKURU Mungu kwa kutukutanisha tena leo. Ametaka iwe ndiyo maana imekuwa. Kama asingetaka, ingekuwa tofauti leo. Kila sifa njema anastahili yeye mlinzi, mlezi na mpaji wa viumbe vyote.

Kuna mambo muhimu ya kujifunza kuhusu furaha yako na amani ya mwenzi wako. Labda kabla sijaenda mbele zaidi, nikufafanulie hili: Sanaa ya busara katika maisha inajumuisha vitu vinne.


Mosi ni malengo, Mungu ana nafasi yake, hatua chanya na mafanikio endelevu. Ukikaribisha busara kama kanuni yako ya kuishi, maana yake unahitaji amani na furaha. Hilo liweke akilini halafu tuendelee.

Ukitaka kuishi kwa busara ni lazima uwe na mtazamo wenye furaha. Unapaswa kuiangalia dunia kwa fikra na macho. FURAHA; Hebu angalia wengine wanavyosononeka kwa kuikosa, kisha jifunze kwa wenye amani.

 Mtu sahihi ni yule anayejifunza kupunguza msongo wa mawazo, Anayejitahidi kuongeza furaha na kupanua uwezo wake. Kama ndivyo, basi unatakiwa ujiulize: “Utapata vipi furaha ikiwa mwenzio amenuna?”

Akiwa amekasirika utaweza kucheka? Jibu ni kwamba haiwezekani na endapo moyo wako una amani wakati mwenzako amejikunja, ni wazi kwamba penzi lenu limejaa mashaka. Je, mtaenda hivyo mpaka lini?

Ni vizuri kila mtu ajifunze kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza furaha. Ukifanikiwa kuiweka chanya furaha ya mwenzi wako na yako itapatikana. Zingatia msemo kuwa ninyi ni kitu kimoja, wewe ni yeye!

Huwezi kuondoa msongo wa mawazo na kukaribisha furaha kama utakuwa unafeli kila siku kitandani. Utajiona mnyonge lakini na mwenzako pia utamtesa. Unakwea lakini ukishuka, utamuacha na ‘ugwadu’ mwilini. Akamalizwe na nani?

Tunahitaji kujielimisha mara kwa mara kuhusu mapenzi. Haina maana kwamba hujui, la hasha! Inawezekana una uelewa mkubwa lakini huwezi kujaliwa utambuzi wa kila kitu.

Hivyo basi, nakushauri mara kwa mara uwe unapita kwenye ukurasa huu ili uchote japo elimu kidogo ambayo kwa maana moja au nyingine inaweza kuwa tiba ya jambo ambalo linakutatiza.

Ipo wazi kuwa wengi wanateswa na mapenzi. Kila mmoja anahitaji amuweze mwenzi wake, badala ya kujenga hisia za kuridhishana. Yaani wewe utamani kumfurahisha na siyo kumkomoa.

Hali kadhalika, naye pia awe na hisia za kukuridhisha. Asiwe na mawazo ya kukuchezesha ligwaride au kukukomoa ili akajisifie. Mapenzi hayapo hivyo, wenye hulka hiyo ni malimbukeni.

Mapenzi ni starehe, siyo mapambano ya ana kwa ana kusema lazima mmoja aibuke mbabe. Hisia hizo ndizo ambazo zinawafanya wengi waumbuke. Wanatumia nguvu nyingi katika tendo linalohitaji nafasi.

Siku zote unapoingia kitandani unapaswa kujiamini. Baada ya hapo chukua muongozo wa kuheshimu hisia za mwenzi wako. Naye pia unatakiwa kumuamini kuwa atakupa kitu kamili. Amini katika matokeo chanya.

Wanasema mkamia maji hayanywi. Kwa maana mtu anayeendekeza kiu na kufakamia maji ili anywe mengi, matokeo yake hata glasi hakumaliza. Alibaki anayatazama kwa jicho la mshangao. Yanemshinda nguvu.

Kuna pointi moja ambayo inawashinda wengi. Inawafanya wasielewe namna sahihi ya kutekeleza tendo pindi wanapokuwa kitandani. Wanakosa kitu cha msingi, “busara ya kitanda”, ni muhimu kujua, kwa maana ina msaada mkubwa.

Itaendelea wiki ijayo.

No comments: