ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 16, 2011

Hayawi hayawi sasa yamekua

Timu ya Bongo Real FC
Timu ya DC Nyalugusu SC

ule mpambano wa kukata na shoka wa marudiano  ulikuakua unasubiliwa kwa hamu na wachezaji wa DC Nyalugusu na Mashabiki DMV,sasa ni Jumapili July 24,2011.


Bongo Real picha ya pamoja baada ya mazoezi

Mechi ya kwanza iliyochezwa June 12,2011 na kuvunjika huku Bongo Real ikiwa mbele kwa goli 3-2,mechi hii ilileta uhasama kati ya timu hizi mbili na kusababisha urafiki wa Luka Kinyang'anyiro  na Liberatus Mwang'ombe kuvunjika kwa wiki kadhaa,kwani Libe alimshutumu Kinyang'anyiro kwa kusababisha mpambano kuvunjika.Huku DC Nyalugusu wakijaribu kuomba mechi ya marudiano na Bongo Real kuwakejeri kuwataka walipe $10,000 Cash ndio waweze kurudiana nao.
DC Nyalugusu SC wakiwa kwenye mazoezi makali

Homa ya mpambano huu umeanza kupanda kwani jana zilionekana Text kutoka kwa kocha mchezaji Jabir Jongo  wa DC Nyalugusu akihimiza wachezaji wake wafike mazoezini.
Adam NY nae ameanza mazoezi rasmi jana na timu yake ya Bongo Real FC

Kwa upande wa Bongo Real FC wao wanaendelea na mazoezi kama kawaida na mzoezi yao ni kila siku isipokua Jumamosi,akithibitisha kuhusu mpambano huu timu kepteni wa Bongo Real amesema wachezaji wapo fiti na wako tayari kwa mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa DMV na vitingoji vyake na sasa ndio gumzo kubwa mitaani.
Said Nassor mchezaji na tajiri wa kununua wachezaji hapa akiwa mazoezini DC Nyalugusu siku chache kabla hajaelekea Bongo kwa likizo

DC Nyalugusu Mazoezi yao yalianza rasmi jana wakijiandaa na kipute cha marudiano mechi itakayochezewa Meadowbrook park saa 11 jioni(5:00pm) huku wakidai Bongo Real FC wanajifanya wajanja wanaita mechi wakati wakijua Libe na Said hawatakuwepo lakini wategemee kipigo kitakatifu kutoka kwa DC Nyaligusu SC
Mchezaji Vincent Ndusilo Bongo Real FC imemkatia rufaa kwamba uraia wake wa Hyattsville unautata

Vingozi wa Bongo Reaf FC wamekata rufaa kwa mchezaji wao Vincent Ndusilo kwamba DC Nyalugusu walidanganya kwamba mchezaji huyo anaishi Hyattsville,uchunguzi umebaini bado mchezaji huyo anaishi Colombia,na sasa swala hilo lipo mikononi kwa chama cha soka DMV ambao nao wameahidi kutoa uamuzi Jumatano July 20,2011 uhalali wa wapi mchezaji huyo achezee.

2 comments:

Anonymous said...

imekuwaje

Anonymous said...

Vicent yupo South America ? Yupo mji gani hapa Colombia ? Bogota ?