ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 15, 2011

Pati ya Yanga Nyumbani Lounge,Lady Jay Dee akabidhiwa uanachama Yanga

Lapa linawakilisha mwananchi wa kawaida, Mzalendo, Mlala hoi
Huyu ndio alieleta maneno yote mjini Asamoah, lile Goli
Captain Shadrack Nsajigwa
Francis Kifukwe na walezi wengine wa Yanga
Mwenyekiti, Lloyd(picha kwa hisani ya Lady Jay Dee Blog)
Na Wilbert Molandi
MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Yanga, Francis Kifukwe, juzi alimkabidhi kadi ya uanachama wa klabu hiyo mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ (pichani) na mumewe Gardner Habashi.

Kifukwe alimkabidhi msanii huyo kadi akiwa na Mwenyekiti aliyepo madarakani, Lloyd Nchunga, kwenye hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo juzi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge uliopo Msasani, Namanga jijini Dar es Salaam.

Katika makabidhiano hayo, Kifukwe aliwashukuru Jay Dee na Gardener kwa kuwaandalia hafla hiyo fupi wachezaji na viongozi wa Yanga kusherehekea ubingwa wa Kombe la Kagame kwa kuwafunga watani wao wa jadi Simba kwa ushindi wa bao 1-0.

Baada ya kuwakabidhi kadi hizo, Kifukwe aliimba wimbo wa taifa pamoja na kuwalisha keki wachezaji wote walioudhuria hafla hiyo wakiwemo Kenneth Asamoah, Davies Mwape, Yaw Berko, Jerry Tegete, Godfrey Bony, Juma Seif ‘Kijiko’, Chacha Marwa, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro, Nurdin Bakari.

Hafla hiyo ilihudhuriwa wasanii wa filamu wakiwemo Steven Kanumba, Ray Kigosi, Jacquline Wolper, Jacqueline Pentzel, Aunt Ezekiel,  Steve Nyerere na Jacob Steven ‘JB’.(Habari kwa hisani la GPL)

No comments: