ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 20, 2011

Shukrani za dhati

Nawashukuru wote walioweza kufika kwenye shower yangu na kufanya shughuli hii ifane pia ningependa kuwashukuru wote waliosafiri umbali mrefu kutoka State mbali mbali kuja kujumuika pamoja nami pia napenda kuwashukuru wale wote ambao hawakuweza kufika japo nia ilikuwepo lakini  kutokana na kutingwa na mambo muhimu ikawalazimu kushindwa kuhudhulia Baby Shower.

Shukrani za pekee ziwaendee waandaaji wa Shower hii na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kwani nia ilikua moja kufanya shower hii ifanikiwe.

Napenda pia kuwashukuru Swahili Villa,Vijimambo,Sunday Shomari kwa kuipamba shower hii kwa picha safi kwenye Blog zenu.

Shukrani za pekee kwa Dj Luke na MC Quize nashukuru sana kwa kazi nzuri.

Sina cha kuwalipa kitakacholingana na mlichonifanyia najua asante halingani hata kidogo na hayo makubwa mlionifanyia kusema ukweli nimeguswa sana nashukuru sana na Mwenyezi Mungu awazidishie. 

No comments: