ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 16, 2011

Twiga kuanza na Ghana Afrika

Image
TIMU ya soka ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) itaanza mashindano ya All Africa Games yatakayofanyika Septemba mwaka huu jijini Maputo, Msumbiji, Septemba 5 kwa kupambana na Ghana.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Twiga Stars ambayo iko kundi B itacheza mechi ya pili Septemba 8 mwaka huu kwa kupambana na Afrika Kusini kabla ya kumaliza hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe. 


Ratiba inaonesha kuwa mechi za nusu fainali zitachezwa Septemba 13 na 14 mwaka huu wakati ile ya kutafuta mshindi wa tatu itakuwa Septemba 16 mwaka huu na fainali ni Septemba 17 mwaka huu.

Timu mbili za kwanza katika kila kundi ndizo zitakazofuzu kwa hatua ya nusu fainali.

Kundi A katika michuano hiyo lina timu za wenyeji Msumbiji, Cameroon, Algeria na Guinea.

Nigeria ndiyo waliokuwa mabingwa wa 2007, lakini hawakufanikiwa kufuzu kwa michuano hiyo mwaka huu ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne.


Habari Leo

No comments: