Waandishi Wetu, Dar, Mikoani
BEI mpya ya mafuta iliyotangazwa juzi na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imesababisha vurugu kwenye soko la bidhaa hiyo nchini baada ya baadhi ya wafanyabiashara kufunga vituo vyao vya mafuta wakipinga huku wengine kuendelea kuuza mafuta hayo kwa bei ya kuruka.
Uchunguzi uliofanywa jana umeonyesha kwamba ni vituo vichache nchini ambavyo vimetii agizo hilo la kuuza. Juzi, Ewura ilitangaza kushusha bei ya petroli kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na asimilia 9.17, dizeli Sh173.49, sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa Sh181.37, sawa na asilimia 8.70.
Katika jiji la Dar es Salaam baadhi ya wamiliki walifunga vituo vyao kwa kamba na wengine walifuta bei katika mbao za matangazo ingawa wengine walitii agizo la kuuza petroli kwa bei ya kikomo ya Sh2,004, dizeli Sh1,911 na mafuta ya taa Sh1,905.

Vituo vyafungwa Muheza
Wilayani Muheza wamiliki wa baadhi ya vituo vya kuuzia mafuta nao walisitisha kutoa huduma hiyo jana. Baadhi ya wafanyabiashara waliohojiwa ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walisema bei hiyo iliyotangazwa na Serikali haina maslahi kwao kwa kuwa bado wanayo akiba ya mafuta waliyonunua kwa bei ya zamani. Wamiliki hao wameiomba Serikali kuwapa muda ili wamalize kuuza mafuta waliyonayo kwani kupunguza bei ghafla ni kuwaumiza kibiashara.
"Hatuwezi kushusha bei mpaka tumalize mafuta tuliyonunua mwanzo kwa bei ya juu kwa kuwa tutapata hasara... tumeambiwa tushushe Sh100 tutakuwa hatuna faida tutafilisika kwani Sh100 katika biashara ya mafuta ni kubwa sana," alisema mmoja wa wamiliki hao.
Wamiliki vyambo vya moto wilayani hapa walionyesha kufurahishwa kwao na punguzo hilo la bei ya lakini wakalalamikia punguzi la Sh100 tu huku wengi wakionekana kutaka bei ya petroli ipungue hadi kuwa Sh1,500 kwa lita. Mgomo huo wa jana ulisababisha ulanguzi mkubwa wa petroli ambayo iliuzwa mitaani kwa Sh3,000 kwa lita moja.
Kigoma bei elekezi yapigwa teke
Uchunguzi uliofanywa jana mjini hapa umeonyesha kuwa mafuta ya taa, dizeli na petroli yanauzwa kwa bei ya juu tofauti na maelekezo ya Serikali ya kupunguza kodi na hivyo kuwaondolewa mzigo wananchi.
Baadhi ya vituo vimeamua kusitisha utoaji wa huduma kwa madai kwamba bei mpya iliyotangazwa na Ewura itawasababishia hasara kutokana na wao kununua mafuta hayo kwa bei ghali.
‘Leo (jana) hatujauza kabisa mafuta hapa na hii inatokana na Ewura kudai bei ipungue, lakini hawa wamiliki wametazama walivyonunua huu mzigo wakaona kwamba kwa bei hiyo mpya, ni lazima watapata hasara, sasa bado wanasikilizia kuona hali inavyokwenda katika vituo vingine,” alisema mfanyakazi wa kituo kimoja cha kuuza mafuta Mjini Kigoma.
Iringa wananchi bado walia bei juu
Baadhi ya wakazi wa Mjini Iringa wamesema pamoja na Ewura kupunguza bei ya mafuta juzi, bado bei hiyo mpya haijawapa nafuu. Wakizungumza jana walisema kwa maisha ya mtu wa chini, bei hiyo mpya ya mafuta iliyotangazwa haijapunguza makali ya maisha.
“Bei bado maumivu hasa haya mafuta ya taa ambayo yanatulenga sisi wa kawaida. Hakuna unafuu wowote vinginevyo mazingira yataendelea kuharibiwa, unadhani nishati tutaipata wapi? Mafuta ndiyo hayo bei juu,” alisema Enock Mfalingunzi, mkazi wa Makorongoni mjini hapa.
Katika baadhi ya vituo vya mafuta Mjini Iringa, bei ya Petroli ilikuwa ni kati ya Sh2,068 mafuta ya taa Sh 1,968 hadi 1,990, dizeli Sh1,975 hadi Sh1,990.
Rukwa wagoma
Mkoani Rukwa wafanyabiashara wa vituo vya nishati ya mafuta wamesitisha utoaji wa huduma hiyo. Jana, sehemu kubwa ya vituo vinavyouza mafuta hayo vilikuwa wazi kwa muda wote lakini havikuwa vikitoa huduma hiyo kwa visingizio mbalimbali ikiwamo ya kuharibika pampu za kusukuma mashine, kukosa umeme na vingine vikidai kutokuwa na mafuta kwa wiki moja sasa.
Karibu vituo vyote vya Sumbawanga Mjini, Nkasi na Mpanda kwa siku nzima ya jana havikuweza kutoa huduma hiyo hali ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji bidhaa hiyo. Kutokana na hali hiyo, walanguzi walikuwa wakiuza kwa bei ya kuruka bidhaa hiyo. Mafuta ya taa yaliuzwa kati ya Sh2,700 hadi 3,000, petroli na dizeli zilifikia kati ya Sh5,000 na Sh6,000 kwa lita.
Baadhi ya watumishi wa vituo hivyo wameeleza kuwa bei iliyotangazwa za Serikali ya lita moja ya petroli kuuzwa Sh2,177 na dizeli Sh2,184 haina manufaa kwa wafanyabiashara hao hivyo wameamu kuendesha mgomo baridi hadi pale mamlaka inayohusika itakaporekebisha tena bei hizo.
Tanga magari yakwama
Madereva wa magari pamoja na pikipiki jana walipoteza muda mwingi kutafuata mafuta katika baadhi ya vituo vilivyopo jijini Tanga kutokana na vingi kuingia katika mgomo baridi vikipinga bei mpya.“Tumekwama, tumeishiwa mafuta na hatuwezi tena kuendelea na kazi, vituo vyote sasa hivi vimefungwa eti ni mgomo baridi wa kupinga kitendo cha Serikali kupunguza bei,” alisema Haji Ali, dereva wa daladala inayofanya kazi kati ya Magomeni na Raskazone.
Dereva huyo alisema jana asubuhi baadhi ya vituo vilikuwa vikiendelea kutoa huduma ya kuuza mafuta kwa bei ya zamani lakini ilipofika saa 8:00
mchana viliacha kuhudumia na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa. Mmoja wa wafanyakazi katika moja ya vituo hivyo alisema wamekatazwa na waajiri kutoa huduma kwa kuwa wamekubaliana kuendesha mgomo baridi.
“Mabosi wetu wametuambia tusiuze mafuta, tunafanya mgomo baridi kwa sababu Serikali imepunguza bei huku kukiwa na akiba ya mafuta ambayo
yalinunuliwa kwa bei kubwa,” alisema mfanyakazi mmoja.
Mbeya nako wagoma
Jijini Mbeya, vituo vingi vilisitisha kuuza mafuta majira ya saa mbili asubuhi jambo ambalo lilitafsiriwa na baadhi ya wakazi kuwa wamiliki waliwasiliana na kuzuia uuzaji wa mafuta kama njia ya kupinga agizo la Serikali.
Baadhi ya madereva wa daladala walisema asubuhi walinunua mafuta kwa bei mpya lakini waliporudi tena mnamo saa 5:00 walishangaa kuambiwa umeme umekatika huku vituo vingine wakidai kuwa mafuta yamekwisha jambo ambalo walisema limewashangaza kwa kuwa na matatizo yanayofanana kwa wakati mmoja.
Wafanyakazi katika vituo vya mafuta ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema tatizo lililojitokeza ni Serikali kutaka kushindana na wamiliki wa vituo vya mafuta jambo lililosababisha wao kuzuiwa kuuza mafuta na kwamba wanasubiri amri ili waendelee na biashara kama kawaida au la.
Akizungumzia mgomo huo baridi, mkazi mmoja wa jiji la Mbeya, Joseph Richard alisema Serikali inatakiwa kuwachukulia hatua kali wamiliki wote wa mafuta watakaobainika kuhusika kwa makusudi katika mgomo huo kwa kuwa hawapo juu ya sheria.

Alisema wameonyesha kuwa na dhamira ya kuwakandamiza wananchi wa kawaida: “Bei ya mafuta ikipanda katika soko la dunia usiku na wao asubuhi wanapandisha bila kujali kama walikuwa na akiba ya muda mrefu ambayo walinunua kwa bei ya chini, lakini Serikali kushusha bei kidogo tu, wanafunga vituo," alisema.
Habari hii imeandikwa na Elizabeth Edward, Timothy Marko; Dar es Salaam. Steven William, Muheza; Tumaini Msowoya, Iringa; Muheza, Anthony Kayanda Kigoma; Mussa Mwangoka, Sumbawanga, Burhani Yakub, Tanga na Brandy Nelson, Mbeya

Mwananchi
No comments:
Post a Comment