ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 14, 2011

BURIANI

Macrina                                           Kidee


Buriani dada zetu, majonzi mwatuachia
Mmetutoka wachanga, tungali twawatamani
Twalia na uchungu , yote mapenzi Mungu
Macrina na Kidee, Mola awalaze pema

Wazazi wetu poleni, yaliyotusibu makubwa
Nyumbani kwetu mbali , ndugu zetu wasubiri
Twajiuliza kwanini, majibu hatuyapati
Macrina na Kidee, Mola awalaze pema

Maisha safari ndefu, wenzetu wamemaliza
Twawaombea kwa mola, pema wapumzike
Wabillah Tawfiq, DMV kwa herini

Macrina na Kidee, Mola awalaze pema

3 comments:

Anonymous said...

abarikiwe alietunga utenzi huu, na Mungu awapokee wapendwa wetu.
tuliobaki tuzidi kushikamana.
Luka ubarikiwe pia

Anonymous said...

Amen, nawe ubarikiwe

Anonymous said...

RIP To you'll. Kidee I remember you vividly from the Waldorf College days. You was a very nice, kind and loving person. I was very shocked when I heard your passing. I believe you are at a better place now. Enough of suffering.