ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 28, 2011

Futari Mji wa Reading

 Baadhi ya Viongozi wa REACO katika Picha ya pamoja
READING EASTERN AFRICAN COMMUNITY(REACO) Iliandaa futari maalum leo jioni 28.8.11 na kuwaalika wanajumuia mbalimbali kutoka  Reading, London, Coventry na sehemu nyingine ili kupata futari kwa pamoja. Hii ni desturi ambayo hufanyika kila mwaka wakati huu wa mwezi mtukufu ramadhani. Lengu kuu haswa ni kujumuika pamoja katika kudumisha upendo, amani na umoja kwa wana jumuia pamoja,kuzingatia yale yote yalio mema na kukataza yalio Mabaya.

Mgeni Rasmi wa siku ya leo alikuwa Mh Naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na baadhi ya maofisa wa ubalozi wetu wa Tanzania Hapa London.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa REACO Said Mahmud tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioitikia mwito na kuja kujiunga nasi. Tunawashuru sana.

Kwa maelezo au mawasiliano zaidi tafadhali tutumie email ifuatayo, reaco@hotmail.co.uk

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE

 Baadhi ya viongozi wa REACO wakipata Futari
 Futari Ikiendela
 Futari ilienda sambamba na kubadilishana mawazo
 Mh Chabaka akifurahia jambo wakati Afisa wa UBalozi Kiondo akiteta na Ustaadhi Sungura 
 Mh Naibu Balozi akipata futari
 Mh Naibu Balozi Chabaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa REACO
 mtoto mwanajumia nae akila futari
 picha ya pamoja na wanajumuia
 wanajumuia pamoja na wageni wakipata Futari kwa pamoja
 wanajumuia wakijiandaa kwa kabla ya kupata futari
watoto wakipata futari

No comments: