ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, August 23, 2011
Gaddafi
WAASI WAZINGIRA TRIPOLI, WATOTO WAKE WATEKWA
TRIPOLI,Libya Aljazeera
BAADA ya mapambano ya miezi sita kutoka mji mmoja hadi mwingine, hatimaye waasisi nchini Libya wameingia mji mkuu wa Tripoli ambako ni ngome kuu ya kiongozi wa nchi hiyo kanali Mummar Gaddafi na hadi jana jioni walikuwa wakidhibiti karibu asilimia 95 ya mji huo.
Waasi hao ambao wamekuwa wakipigana nyuma ya vikosi vya kijeshi vya Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato) katika siku hiyo ya kwanza kuingia Tripoli, wameweza pia kukatamata watoto wa tatu wa Gaddafi ambao ni pamoja na Saif al-Islam, Mohammed Al Gaddafi ambaye ni mtoto mkubwa na Saad, lakini kiongozi huyo akiwa hajulikani aliko.
Mbali ya kukamata watoto hao, waasi pia wamefanikiwa kukamata makao makuu ya Kituo cha Telivisheni ya Taifa ya nchi hiyo na maeneo muhimu. Gaddafi ajichimbia mafichoni Hata hivyo, Gaddafi ambaye aliapa kutoweka silaha chini dhidi ya waasisi hao na Nato aliowafananisha na samaki wa bahari ya Meditarranean, hadi jana jioni hakuwa akijulikana aliko.
Jioni, Kanali Gaddafi alinukuliwa na kituo cha Aljazeera akiwataka raia wa Libya kujitokeza na kuukomboa mji wa Tripoli. Mwanamapinduzi huyo alisisitiza, '' Jitokezeni, jitokezeni niko nanyi, msirudi nyuma, tutapigana hadi kuikomboa nchi yetu kuzuia uthibiti, msiwakubalie wanyakuzi kuiteka nchi yetu, nitapigana pamoja nanyi kama nilivyoahidi''.
Kiongozi wa waasi afanya mkutano na waandishi Jana mchana, kiongozi wa waasi Mustafa Abdul Jalil na mwenzake wa Baraza la Taifa la Mpito (NTC), katika mkutano wao na waandishi wa habari walisema bado hawakuwa wameweza kudhibiti eneo aliliokuwa akiishi kiongozi huyo. Alisema, hakuwa akijua kama Gaddafi alikuwa katika ngome yake au la na kuongeza kwamba, "hatujui kama Gaddafi bado yuko pale au ameondoka nchi ya Libya."
Hadi jana jioni Gaddafi aliaminika kujificha katika mji wa Bab al-Azizia ambao ni ngome yake kuu na hata waasi, wamekuwa hawana uhakika kama alikwishaondoka au la kwani walikuwa hawajaufikia mji huo. Nato yatangaza kushirikiana na serikali ya waasi Katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, alisema jumuiya hiyo iko tayari kushirikiana na baraza la kitaifa la mpito linaloongozwa na waasi.
Juzi Picha za televisheni zilionyesha waasi wakiwa katika uwanja wa Green Square uliopo mji mkuu huku makundi ya watu wenye furaha wakisherekea kuwasili kwa waasi hao katika uwanja huo.
Serikali ya Libya ilisema takriban wanajeshi 65,00 watiifu kwa kanali Gaddafi wamebakia mjini Tripoli lakini ni wachache tu walioonekana wakati waasi walipokuwa wakielekea kuuteka mji huo. 1,300 wauawa katika mapambano Tripoli Msemaji wa serikali ya Libya , Mussa Ibrahim, alisema takriban watu 1300 wameuwawa mjini humo katika mapambano kati yao na majeshi ya kiongozi huyo baada ya kuingia mjini humo.
Obama: Gaddafi yuko ukingoni Rais wa Marekani, Barack Obama alisema utawala wa Gaddafi umefikia ukingoni na kumtaka ajisalimishe ikiwa ni pamoja na kuondoka madarakani ili kuepusha damu zaidi kumwagika. Obama mbali ya kumtaka Gaddafi kuachia ngazi kuepusha umwagaji damu zaidi, pia aliwataka waasi kuheshimu haki za binadamu, kuonyesha uongozi mzuri, kuhifadhi taasisi za Libya na kuelekea katika demokrasia.
Misiri yatambua waasi Tayari viongozi mbalimbali duniani wamemtaka Gaddafi kuachia madaraka huku Misiri ikitangaza rasmi kutambua waasi kama serikali halali.
Mapambano yanaendelea Ripoti za hadi jana jioni zilisema kulikuwa na mapigano makali ambayo yalisababisha milioni ya bunduki na milipuko katika viunga vya mjio huo mkuu.
17 Feb:Maandamano dhidi ya Serikali kuanza Nchini Libya 24 Feb - 6 Mar: Waasi kudhibiti maeneo kadhaa ya miji nchini Libya
17 Mar:Ndege za umoja wa Mataifa (UN)kuruka katika anga ya Libya kwa lengo la kulinda wananchi. 30 Mar: waziri wa mambo ya nje Moussa Koussa atoa kasoro Mapambano ya waasi dhidi ya Gaddafi Mapambano ya waasi dhidi ya Gaddafi yalianza Februari 17, baada ya kufanya maandamano kupinga utawala wake kipindi ambacho tayari serikali za Tunisia na Misri zilikwishang’olewa kwa mtindo huo.
Gaddafi ni nani?
Kanali Gaddafi ni kiongozi pekee aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na katika Nchi za Kiarabu. Ameongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu akiwa na miaka 27.
Ni mwanasiasa mashuhuri hakuna shaka lolote kuhusu hilo. Ni mwanasiasa anayeweza kuhimili misukosuko ya kisiasa kwa hali ya juu sana. Muammar alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942. Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri Gamal Abdel Nasser, wakati alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel katika mgogoro wa kugombea mfereji wa Suez mwaka 1956.
Alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani katika mji Benghazi, na kupanga mapinduzi ya Septemba mosi mwaka 1969. Gaddafi alianza kujenga itikadi zake za mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake kinachofahamika kama Kiijani Kibichi kwa Kiswahili.
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari. Mwaka1977, aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambaLo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Mfumo huo ulivuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine ya kijamii na kiusalama. Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment