Advertisements

Tuesday, August 30, 2011

Natamani mfungo wa Ramadhani uendelee!

Wallah natamani mfungo uendelee. mume wangu kiranga kitupu haishi hodi hodi vijumbani. Ramadhani yote mume amekuwa mwadilifu na mwenye mapenzi bashasha, leo Ramadhani imekwisha moyo unanienda mbio, mume haishi vikao vya harusi na kulala matangani.  

Nimejitahidi kila kona kumdhibiti Bwana huyu bado sijafanikiwa; walimwengu nisaidieni  raha ya mume sina si kana kwamba simpendi mume wangu la hasha nampenda kwa mapana na marefu. Hodi hodi vijumbani zitakwisha lini? Mwezi mzima huu sikusikia nimechelewa kwenye kikao cha harusi wala nimelala kwenye matanga ya watani. 

Kila siku namuomba Mungu atunusuru sijui balaa hili litakwisha lini, ninauhakika safari ya Igunga kwenye kampeni za uchaguzi ipo njiani. Wapwani walisema mla mlaleo mlajana kala yani?
Nawatakia Eid njema,
 
Bilhuda Omar Abbas

No comments: