Shirika maarufu la kutoa msaada la Oxfam linasema serikali na wafadhili hawachukui hatua haraka kukabiliana na matatizo ya ukame katika kanda ya pembe ya Afrika.
Shirika la Oxfam lenye makao yake London lilisema Jumanne kwamba wafadhili lazima watimize haraka ahadi walizotoa kusaidia zaidi ya watu nusu milioni ambao wanakabiliwa na hatari ya nja nchini Somalia, Kenya na Ethiopia.
Shirika la Oxfam lenye makao yake London lilisema Jumanne kwamba wafadhili lazima watimize haraka ahadi walizotoa kusaidia zaidi ya watu nusu milioni ambao wanakabiliwa na hatari ya nja nchini Somalia, Kenya na Ethiopia.
Oxfam inasema inataka kusaidia jumla ya watu milioni 3 lakini inakabiliwa na upungufu wa dola milioni 55 kwenye mipango yake.
Ombi hilo limetolewa siku moja baada ya Umoja wa Afrika ulipotangaza utaanda mkutano wa viongozi wa wafadhili mjini Addis Ababa wiki ijayo kuchangisha fedha kwa ajili ya zaidi ya watu milioni 12 walioathiriwa na ukame.
Umoja wa Mataifa karibuni ulitangaza baa la njaa katika maeneo mawili ya Somalia kusini na inaonya kwamba hali ya baa la njaa inaweza kusambaa kuelekea maeneo mengine. Umoja wa Mataifa wiki iliyopita ilitoa ombi la msaada wa dola bilioni 1.4.
Ukame umelazimisha maelfu kwa maelfu ya wasomali kuzikimbia nyumba zao kwenda kutafuta chakula na maji. Wengi wao wamekwenda kwenye makambi mjini Mogadishu huku wengine wamekimbilia kwenye makambi ya wakimbizi ambayo tayari yamejaa nchini Kenya au Ethiopia.
No comments:
Post a Comment