Wednesday, August 31, 2011

Uingereza yapeleka dola bilion 1.6 Libya-BBC

Ndege ya kijeshi ya Uingereza imepeleka pauni milioni 950 Libya baada ya Umoja wa Mataifa kuondoa tanji iliyokuwa imelengwa kwa Kanali Gaddafi.
Noti, zilizotimia dinari za Libya bilioni 1.8 zilizochapishwa Uingereza, zitawasilishwa kwenye benki kuu ya Libya.
Afisa mmoja amesema fedha hizo zinatakiwa ziwepo ili ziingizwe kwenye mashine ya kutolea pesa yaani ATM na kusambazwa kwenye benki haraka iwezekanavyo.
Afisa huyo alisema fedha hizo zitasaidia kulipa wafanyakazi wengi wa sekta ya umma wakati wa likizo ya Eid.
Wengi ambao wanategemea mishahara ya serikali hawajalipwa katika kipindi cha wiki kadhaa.
Hatua hiyo inachukuliwa siku moja kabla ya mkutano mkuu wa kimataifa juu ya hatima ya Libya unaotarajiwa kufanyika mjini Paris siku ya Alhamis.
Mkutano huo utaongozwa kwa pamoja na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.

No comments: