ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 21, 2011

LEO NDIO LEO ASIYE KUWA NA MWANA AELEKE JIWE


Ule mpambano wa kukata na shoka unaosubiliwa kwa hamu na wakazi wa DMV na vitongoji vyake hatimae zimebaki saa chache kindumbwe ndumbwe kianze.

Mechi hii iliyokua imetawaliwa na majigambo takribani wiki nzima hatimae leo itafikia tamati.

Mechi itaanza saa 9 kamili(3pm sharp) na itakua ya dkk 20 kila upande,Wazee ambao wao walishindwa kutaja kikosi wiki iliyopita sasa wameweka kikosi chao wazi.

Akizungumuza na Vijimambo kwa njia ya simu Kepteni wa Timu ya Wazee DC Mzee Muganda amesema wachezaji wake wako fiti na wapo tayari kwa mchezo isipokua Nuru Omar anaesumbuliwa na kifundo cha mguu lakini wachezaji wengine wapo tayari na wamejigamba wataondoka na ushindi mnono.

Mzee Muganda amesema anatarajia kushusha kikosi cha mauaji,Golikipa atakua Phanuel Ligate akisaidiwa na beki wa kulia Edgar Tibaikweitira,beki wa kushoto atakua Ayub Mansour,4 atacheza Ally Bambino,5 Elius Magembe,6 Idd Sandali,7 Kessy Janabi,8 Said Mateso,10 Mzee Muganda,Saidi Mwamende au Nuru Omar kama atajisikia vizuri.amesema wachezaji wengine ni Marco Mbullu,David Barcelona na ameomba wachezaji wote Wazee wanao taka kucheza wafike mapema.

Mzee Muganda alisema,tunasikitika kuwakosa wachezaji wetu watatu hatari ambao kwa sasa wa likizo Tanzania,prof Boas,Mzee Kasembe,Hamza Mwamoyo na Mzee Kalala.

Nae timu kepteni wa Ubalozi Colonel Maganga amesema kikosi chake kipo imara sana na haya ndio alizungumuza jana


na alisema kikosi chake ni kilele isipokua Edward Masanja ni majeruhi.

Mechi itachezewa
  Bohrer Park (Water Park) Pavilion Shelter - Picnic Area
506 S. Frederick Avenue
Gaithersburg, MD 20877

Mgeni Rasmi ni Mh Balozi Maajar pia kutakua na nyama choma na vitafunio,
mbali na mpira wa miguu pia kutakuwepo na michezo mbali mbali kama vile kukimbia na magunia,kuvuta kamba na kadha wa kadha

Karibuni wote wakazi wa DMV na Vitongoji vyake

Muda ni kuanzia 8 mchana(2pm) mpaka i usiku(7pm)

Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzie.

1 comment:

Anonymous said...

Lucas kwa nini .una hasira na mimi .sio vizuri.na mungu apendi.cha muhimu kuombeana.angalia watu wanavyokufa.,mtu ujuwi ya leo wala ya kesho.tuwe na amani..mungu akutie .nguvu na siku njema.