Meya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi
Dk. Masaburi awashupalia kuhusu mali za Jiji
Awaambia atachunguza mikataba yote mibovu
Machinga Complex, DDC navyo kuchunguzwa
Awaambia atachunguza mikataba yote mibovu
Machinga Complex, DDC navyo kuchunguzwa
Meya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi amesema uchunguzi kuhusu ubadhilifu wa mali za jiji utaendelea na kutamba kuwa hakuna mtu wa kumzuia.
“Nimeanza na sitaishia hapa eti kwa kuwaogopa, ninapozungumza na wewe narudi jijini kuanza kazi ya kuchunguza mikataba yote mibovu mimi mwenyewe, sitotumia kamati kama huko nyuma,” alisema.
Dk. Masaburi alisema hayo alipozungumza na NIPASHE Jumapili kwa njia ya simu akiwa njiani akitokea Arusha kuja Dar na kusisitiza kuwa atafanyia uchunguzi miradi yote ili kuanika madhambi yote yaliyofichwa.
Alisema kitu kinachofanywa hivi sasa na wabunge wa Jiji la Dar es Salaam, wakiongozwa na Abbas Mtemvu na Mussa Zungu ni kumtisha ili asiendelee kuchunguza maovu, kitu ambacho alieleza hakitamzuia.
Alisema, katika uchunguzi huo hataihusisha kamati ila ataufanya yeye mwenyewe kwa kushirikiana na wataalam mbalimbali wenye utaalamu wa kubaini wizi ndani ya mikataba.
Alitaja miradi itakayochunguzwa kuwa ni pamoja na Machinga Complex, Shirika la Maendeleo jijini Dar es Salaam (DDC) na uuzwaji wa mashamba ya jiji yaliyopo Ruvu na Mpiji Majohe.
Machinga Complex Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Ilala, Zungu na DDC inaongozwa na Mbunge wa Temeke, Mtemvu.
“Nafahamu baadhi ya wabunge wanahusika na ufisadi huu wa mali za jiji, ndio maana wanatafuta visingizio vya kuning’oa lakini watambue hapa wamegonga mwamba,” alisema.
Alieleza anashangazwa na wabunge hao kung’ang’ania kuwa ajiuzulu wakati mikataba yote iliyoingia na Shirika la Usafiri jijini (UDA) hakuwepo na wabunge hao ndio waliohusika katika kujadili mikataba hiyo kupitia vikao vya Baraza la Madiwani.
Hata hivyo, alisema kazi ya kukusanya nyaraka maalum pamoja na idadi ya miradi imekamilika na kilichobaki ni utekelezaji.
Hivi karibuni wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mtemvu walizungumza na waandishi wa habari na kueleza kusikitishwa kwao na tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria na kanuni na taratibu za kulinda maslahi ya wananchi yaliyofanywa na Meya huyo pamoja na Mkurugenzi wa UDA Bakari Kingobi kujiuzulu nafasi zao.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment