
Watu 10 wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, baada ya basi la Grazia kupinduka katika eneo la Mwidu katika barabara ya Dar es Salaam-Morogoro, mkoani Pwani.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Salehe Mbaga, aliliambia NIPASHE jana jioni kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9:20 alasiri baada ya basi hilo lililokuwa likitoa Njombe, mkoani iringa kwenda dare s Salaam kupinduka wakati likijaribu kulipita gari lingine.
Mbaga alisema waliofariki ni wanawake saba na wanaume watatu. Miongoni mwa majeruhi ni wanawake wanane na wanaume 11.
Alisema kuwa majeruhi walikimbizwa na kulazwa katika Hospitali Teule ya Tumbi.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi. Alisema basi hilo baada ya kulipita gari lingine lilikosa mwelekeo na kwenda porini kisha kugonga miti na kusababisha vifo na majeruhi.

Wananchi wa eneo hilo la Mwidu wakiangalia na wengine wakisaidia watu waliopatwa na ajali kwa picha zaidi za ajalia hiyo Bofya Hapa
No comments:
Post a Comment