Thursday, September 1, 2011

Chanzo cha usaliti, jinsi ya kuepuka kusalitiwa na kumgundua anayekusaliti!

Namshukuru Mungu kwa kunijalia fursa hii adimu ya kuzungumza nanyi wapenzi wasomaji wa safu hii ya Mashamsham. Jamani mambo vipi? Sikukuu ya Idd vipi? Natumaini mambo bambam au siyo?

Haya karibuni tena kwenye ‘mambo yetu yalee’ ya malavidavi, si unajua bila mapenzi hakuna maisha?  Huo ndiyo ukweli, huwezi kuishi kama jiwe au mti. Raha ya maisha ni kuwa na mwenzi, mpenzi wa kumpenda na kukupenda kiukweli na siyo kujaribu au kuzuga.


Mpenzi msomaji wangu, nimedhamiria kuzungumzia mambo makuu matatu. Chanzo cha wapenzi kusalitiana, jinsi ya kuepuka kusatiwa na unavyoweza kumgundua anayekusaliti.

Kimsingi hakuna kitu kinachoumiza katika uhusiano wa kimapenzi kama kusikia mpenzi wako anatembea na mtu mwingine tena ambaye huenda unamfahamu, inauma sana.

Ndiyo maana katika makala zangu nyingi huko nyuma nimekuwa nikieleza kwamba, unapobaini mpenzi wako ana uhusiano wa siri wa kimapenzi na mtu mwingine, muache haraka bila kujali maumivu utakayoyapata. Hakuna sababu ya kuvumilia katika hili na kama utaamua hivyo, utakuwa unalikuza donda ambalo litakuja kukuliza siku moja.

Kwa kifupi kasi ya kusalitiana kwa wapenzi imekuwa ikiongezeka kila kukicha kiasi kwamba, unapoingia katika uhusiano unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa. Hii ni kwa sababu watu siyo waaminifu kabisa kwa wapenzi wao.

Unaweza kuwa na mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakuambia hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe katika shida na raha lakini cha ajabu huyo huyo siku moja unaweza kuja kumfumania akiwa na mtu mwingine.

Katika mazingira hayo ni lazima utaumiza kichwa kujua sababu iliyomfanya akakusaliti. Je, ni kutokana na mapungufu yako mnapokuwa faragha? Je, penzi unalompatia hatosheki nalo au amerogwa? Utajiuliza maswali mengi na mwishowe usipate majibu.

Mimi nimejaribu kufanya utafiti na kubaini mambo mengi ambayo yamekuwa chanzo cha wengi kutoka nje ya uhusiano wao. Unaweza kumpa kila kitu, unaweza kujitahidi kumfurahisha kwa kila namna lakini bado kwa sababu hizi nitakazozitaja, unaweza kushangaa unasalitiwa.

Kwanza kabisa imebainika kuwa, tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi watu kushindwa kujizuia kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu, akatokea mwanaume na akamhakikishia kumpatia kila anachotaka, anakubali mara moja bila kukumbuka kuwa ana ‘mtu’ wake.

Mbaya zaidi sasa ni kwamba, wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti.
Hili si kwa wanawake tu, hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.

Ukiacha hilo, tabia zisizoridhisha ni sababu nyingine inayowafanya baadhi ya watu kusalitiana. Wapo ambao wanaishi maisha ya ajabu sana, yaani wanaishi katika ndoa au uhusiano wa kawaida lakini hawaaminiani. Kila mtu anakuwa na wasiwasi juu ya mwenzake.

Afadhali sasa iwe kutokuaminiana tu lakini wapenzi wanakuwa hawasalitiani. Kuna wale ambao ni wazi hawatulii katika uhusiano wao, yaani matendo yao tu yanaonesha wazi kwamba, uaminifu ni sifuri.

Kuwa karibu sana na watu wa jinsi tofauti na kuwa na mawasiliano nao ya siri au mwanamke anapomuwekea mumewe vikwazo katika tendo la ndoa anatarajia akafanye na nani kama siyo kumwambia kutafuta wengine nje?
Ndiyo maana wanaowanyima unyumba waume zao hata wanaposikia wanasalitiwa, wanakosa nguvu ya kuwashutumu wapenzi wao, utamshutumuje wakati wewe humtimizii mambo f’lani?

Itaendlea wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

1 comment:

Anonymous said...

samahani naomba kuuliza mwanamkke kupatiwa anachootaka inaamaana in material sense? wengi twaweza kujipatia mahitaji yetu sidhani kama hili ni tatizo ila nachoona ni kwamba wanaume wanasahau kwamba mwanamke anahitaji affection na bila hiyo hata tendo la ndoa inakuwa ngumu a real woman needs a man by her side not buying her materials but being there and help her pick up eg. clothes and let her know how good she looks in them, or how much she turns him on ,how much he misses her hii inamfanya mwanamke afeel the connection.Vile vile mwanamme ajue kubalance Work,Soccer,Gym and TV time, a woman wants to be given importance in a man's life and not as a mattress when bed time comes. I f a woman does not get affection yes she will have male friend that makes her feel validated and as for now i dont think that is cheating.A women is not to be hanged in the house a as a curtain and be pulled when the sun is down. Man needs to know this, we make effort and they should too.