ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 12, 2011

Kama unapenda kutengeneza mobile apps



Kama ulikuwa unafikiri kwamba itachukua muda kwa HTML5 kutumika zaidi kwenye mobile app basi unajidanganya. Ukweli ni kwamba HTML5 imekubalika na wataalam wengi wa IT duniani kote kama standard kutenegeneza mobile apps. Hii ni kwasababu HTML5 tayari ni web-based standard, tofauti na language nyingine. Application programs nyingi zina uwezo wa kufanya kazi vizuri kwa kutumia browser ambayo imeandikwa kwa kutumia HTML5.
Faida kubwa ya kutumia HTML5 ni developer anaweza kutengeneza HTML5 app inayoweza kufanya kazi kwenye simu yoyote ya mkononi yenye browser nzuri. Hii itaondoa lile tatizo lililopo kwamba app iliyotengenezwa kwa ajili ya platform za simu kwa mfano Android haiwezi kufanya kazi kwenye platform nyingine kwa mfano iOS. Kwa kutumia HTML5 hili tatizo litakuwa halipo tena.
Hadi sasa Linkedln na Pandora zimeshaipitisha HTML5 kama standard ya kutengeneza applications zake. Miaka kadhaa iliyopita Steve Jobs wa Apple alitabiri kwamba HTML5 kuwa standard ya web apps. Apple waliamua kuipa kisogo  Adobe Flash kutoka kwenye platform ya iOS. Kwa sababu Adobe Flash ni plug in application, kumekuwa na shida kwa wengi kutumia application kama You Tube ambayo inatumia Adobe Flash. HTML5 imeondoa tatizo hili, huhitaji tena Adobe Flash kwa sababu una uwezo wa kutumia video moj kwa moja.
Tatizo linaloikwamisha HTML5 kwa sasa ni jinsi program hii itaweza kuuungana vizuri na simu za mkononi zilivyotengenezwa ili kuhakikisha inatumia features zote zilizopo. Hiiinahusiana na features kama kamera, global positioning system (GPS), n.k. Ikumbukwe kwamba application za kawaida za simu zinahusiana vizuri na software ya simu kama vile Android. Hii iniwezesha application hiyo kujenga uhusiano na hardware yenyewe inayoiwezesha kutoa huduma mbali mbali kwa mfano kujua mteja alipo, kutoa direction kwa kutumia ramani, n.k
Kuna mengi mazuri ya HTML5 yanakuja hivyo usiisahau kwenye vitu unavyotakiwa kuvijua japo kidogo

Kutoka blog ya teknolojia :
 http://it4dev.blogspot.com/
Changia mawazo yako

No comments: