ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 9, 2011

Kanali Gaddafi akanusha kukimbilia Niger-BBC

Aliyekuwa Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amekanusha taarifa za uvumi kuwa amekimbilia nchi jirani ya Niger, na kuziita ni uongo na vita ya kisaikolojia.
Alikuwa akizungumza kwa simu kutokea Libya na televisheni moja inayomuunga mkono nchini Syria.
Mapema, Niger ilisema inatafakari cha kufanya iwapo ataomba hifadhi nchini humo.

Maafisa wanasema benki kuu imeuza tani 29 za dhahabu, sawa na dinari milioni 1.7 ($ 1.4 bilioni, £ 875 milioni) wakati bado ikidhibitiwa na na Kanali Gaddafi.
Akiba hiyo iliuzwa kwa wafanya biashara wa wenyeji kati mwezi April na Mei na fedha hizo zilitumika kulipa mishahara, maafisa wa utawala wa muda wa Baraza la Mpito (NTC).
Mazuo hayo yanawakilisha asilimia 20 ya akiba yote ya dhahabu ya Libya, govana wa muda wa Benki hiyo Qassim Azzuz aliwaambia waandishi wa habari mjini Tripoli.
Hakuna mali yoyote isiyohamishika ambayo ‘haionekani au kuibwa’ wakati wa miezi sita ya machafuko na vita ambayo imemuondoa Kanali Gaddafi madarakani, Bw Azzuz alisema, lakini hesabu hiyo haikujumlisha mali iliyokuwa mikononi mwa familia ya Gaddafi.
Baraza la Mpito (NTC) linasema watu walioshuhudia nchini Niger wanaripoti kuona kiasi cha dhahabu na fedha katika msafara uliovuka mpaka na Libya siku chache zilizopita.
"Ikiwa hilo lilitokea, tunataka fedha hizo zirudishwe " Afisa mmoja wa NTC Fathi Badja alisema akinukuliwa na shirika la habari la AFP.
Niger itaambua baadaye iwapo itamkubali Kanali Gaddafi au imkabidhi kwenye mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa Kivita The Hague, waziri wa mambo ya nje ameiambia BBC.
Kumekuwa na uvumi kuwa Kanali Gaddafi anaweza kwenda Niger baada ya kundi linalomuunga mkono kukimbilia huko siku za karibuni.
Baraza la Mpito nchini Libya limeiomba Niger kutomkubali Kanali Gaddafi.
Niger inaitambua mahakama ya ICC, ambayo inatafuta kumkamata Kanali Gaddafi, mwanawe Saif al-Islam, na mkuu wa zamani wa usalama Abdullah Sanussi.
Kanali Gaddafi amekiambia kituo cha televisheni cha Arrai kilichoko Damascus nchini Syria, hakukuwa na kitu kisicho cha cha kawaida kuhusu msafara ulioingia Niger.
Hata hivyo, katika mahojiano na BBC Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger Mohamed Bazoum alikiri kuwa maafisa wa serikali ya zamani ya Gaddafi ni kati ya watu waliovuka mpaka kuingia Niger katika misafara mitatu, lakini Kanali Gaddafi wala watoto wake hawakuwemo katika msafara huo.

No comments: