Monday, September 5, 2011

Kila mtu anazungumzia Cloud Computing. Ni nini hasa? Je, ni kwa watu...

Kwa muda mrefu sasa komputa zetu za nyumbani au makazini zimekuwa ndiyo namna ya kuhifadhi na kutumia mafaili na programs yingine mbalimbali, wakati Internet ni mahali tunapojipatia information zote (rich resource for information) na kuwasiliana. Kitu ambacho kimekuwa kikifanya kazi tofauti kwa wakati wote huu ni services kama Gmail, Hotmail, Yahoo, n.k. Service hizi zinahifadhi data zetu mahali pengine hivyo unapotaka kuona email uliyotumiwa na bosi wako, unakwenda online na kufungua account yako kuion. Huu ni mfano mzuri wa hii service mpya inayoitwa ‘CloudComputing’ au ‘Web 2.0’ au ‘Software as a service
Kwa sasa applications nyingi ziko online na unazitumia kwa kupitia web browser. Kwa mfano picha zako, database za kampuni, n.k.


Cloud Computing na faida zake ni nini?
Kwa urahisi kabisa cloud computing ni kitendo cha kuhifadhi data au applications zako kwenye server maili kadhaa kutoka ulipo wewe. Kila unapotaka kuzitumia unaingia kwenye Internet na kuingia kwenye account yako na kuzikuta hapo. Hakuna haja ya kuzihifadhi kwenye komputa yako, unakuwa unazipata na kuzitumia pale unapozihitaji tu siyo tu kwa kutmia komputa bali kwa kutumia kifaa chochote kama simu, tablets, notebook, n.k. Hii inamaanisha una uwezo wa kuzitumia data zako wakati wowote na mahali popote ulipo.

Watu wengi na makampuni mengi yanajiingiza kwenye mfumo huu kwa sababu ya urahisi wake. Kwa kutumia cloud computing hauhitaji tena komputa yenye storage capacity kubwa sana nyumbani kwako, kumbuka data zako zinahifadhiwa mahali pengine kabisa. Hii inaleta urahisi kwa sababu hununui komputa ya ghali sana. Pia kumbuka komputa inatumia umeme hivyo unakuwa unatumia umeme mdogo zaidi kama uko kwenye cloud ukilinganisha na mtu anayehifadhi kila kitu kwenye system yake nyumbani. Kwa makampuni gharama za kunnua hardware zinapungua sana.

Ubaya wake
Japokuwa tunayazungumzia mazuri ya cloud computing, si kweli kwamba basi tusahau mfumo tuliouzoea wa kuwa na komputa na kila kitu ndani yake nyumbani kwako. Ukweli ni kwamba unahitaji Internet connection kila mara unapotaka kutumia data zako au applications services. Hii ni mbaya kwa nhi kama za kwetu Africa ambapo kuna matatizo ya Internet na umeme.
Tatizo lingine kubwa ni data security. Wakati makampuni mengi yanayohifadhi data zetu kwenye serves zao wanatuhakikishia kwamba watazihifadhi data zetu vizuri, usalama wake ni mdogo kwa maana anayezihifadhi ni mtu mwingine na wala huwezi kugundua ikiwa atazitumia au kuziangalia data hizo bila ruhusa yako. Hii ni hatari zaidi kwa makampuni kwa maana siri zao za kibiashara zinakuwa zinahifadhiwa na mtu mwingine mahali pengine.

Ushauri
Ni vizuri kama tunataka mafanikio, kuhakikisha kabla ya kujiingiza kwenye teknolojia hii, basi tunajua faida na madhara yake. Elimu ya teknolojia hii itakusaidia kufahamu kama unahitaji clod computing kwa matumizi yako au ya biashara yako. Kuna wale wanaopendelea urahisi wa kuweza kuzi-access data zao wakati wowote na mahali popote (flexibility and mobility) lakini wapo wale wanaopenda kuwa na uhakika kwa kuhifadhi data zao wenyewe (ownership and control).
http://it4dev.blogspot.com

1 comment:

Anonymous said...

Great stuff, thank you buddy