Monday, September 5, 2011

ADHA APATAYO MPIGA PICHA

"Ngoja niutengeneze unywele huu"
"We mpiga picha vipi tumekuambia subiri dkk moja"
"Tupe Dkk moja"
"Haya sasa tupo tayari"
Tunapenda kuzipiga hizi picha lakini wakati mwingine yanayotukuta ni siri ya mpiga picha.

Wakati mwingine unampiga mdau picha akiziona anakuambia delete sijapendeza,wadau wengine hukufuata mapema ukinipiga picha nitakufungulia mashitaka,wengine wanataka kulipwa.

Wadau wengine wanakusubili uweke picha zao kwenye blog halafu wanakutumia ujumbe ondoa picha yangu,wakati mwingine mpiga picha unajiuliza mdau kama huyu kama hataki picha yake iwekwe kwenye blog kwanini kapozi kwa madaha na majidai yote haya.

Wadau wengine watapozi kwenye picha na baadae kukupa wakati mgumu wa maswali,kwamba picha yake unaipeleka wapi,utaanza kujieleza "ooh nina blog" atakuuliza tena blog yako inaitwa nini "inaitwa VIJIMAMBO" Vijimambo ndio nini na halafu anataka umtafusilie kwa kimombo inapofikia hapo sasa ndio inakua ngumu unaanza kutafuta neno sahihi upati mwishoe unaishia kumwambia "VIJITHINGS"

Wadau naomba msaada wa hili neno la Vijimambo kwa kimombo maana yake kusudi inisaidie niweze kumpiga picha mdau huyu.

Napenda kuwashukuru wote wanaotoa ushirikiano na wanaofanya kazi ya mpiga picha inakua rahisi

Asante siku njema,
Mpwa

No comments: