Monday, September 5, 2011

Kwa wanajumuiya wote na mrafiki

Kwa niaba ya uongozi wa UTNC napenda kutanguliza shukrani za dhati mno kwa ushirikiano mkubwa mlioutoa kwa kufanikisha brunch na gala. Kwa hakika shughuli zilifana mno, na mnastahiki pongezi za hali ya juu kwa kazi kubwa iliyowakuta. Bila ushirkiano wenu bila shaka hadithi zingekuwa nyingine. Michango mingine inawezekana isionekane machoni mwa wengi,na bado ikawa ni michango mikubwa. Kwa mfano; Aunty Edna hata alivimba miguu kwa kusimama muda mrefu kwa ajili ya mpishi,Dada Talkia alichukua hoteli siku mbili kwa ajili ya kuweza kushiriki vilivyo.
 
Kuna mengi walifanywa na wengi tu ambayo ni makubwa, lakini hayaonekani haraka. M/Mungu awazidishie mioyo ya imani na upendo na tuendelee kushikamana kwa mazuri na yenye manufaa kwa wengi.
Naamini bila shaka kasoro nyingi tu zilikuweko katika harakati za kukamilisha ghafla mbili hizi, japo mimi binafsi sijaziona. Naamini makosa hayo si ya makusudi ila kwa harakati za kufanya bora zaidi. Natanguliza kumradhi kwa makosa yaliyojitokeza .
 
La zaidi;Uchaguzi ni mwezi wa October. nakusudia kutuma pendekezo la Wajumbe wa Kamati ya uchaguzi. likipita,nitawatangazia nyote.
Nawashauri muanzekufikiria na kutafutawagombea wa uongozi wa UTNC. Nafi zitakazowachwa wazi ni; Nafasi ya Mwenyekiti,Katibu,Katibu Msaidizi,Mweka Hazina,Mweka hazina msaidizi na nafasi za Wajumbe wa bodi.
 
Tena, shukrani za dhati kwenu nyote
 
Nassor Ally,Chairman
UTNC & TCLA
P.O.Box 52531
Durham,NC 27717

No comments: