ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 8, 2011

USIKU WA MAADHIMISHO YA MIAKA 189 YA UHURU WA BRAZIL

 Balozi wa Brazil nchini Francisco Luz akihutubia wageni waalikwa katika Usiku wa Maadhimisho ya miaka 189 ya Uhuru wa nchi hiyo,  Maadhimisho hayo yamefanyika Nyumbani kwa Balozi usiku wa kuamkia leo ambapo wageni mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mabalozi na Viongozi wa Serikali ya Tanzania.
 Juu na chini ni Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini risala ya Mhe. Balozi wa Brazil Francisco Luz wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 189 ya Uhuru wa Brazil iliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Ulifika wakati wa kupiga picha za pamoja na kusalimiana kati ya maafisa Ubalozi na wageni mbalimbali.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo
 Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz akibadilishana mawazo wa wakilishi mbalimbali waliohudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 189 ya Uhuru wa nchi hiyo nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam ambapo alisisitiza ushirikiano wa dhati kati ya nchi hizi mbili.
 Maafisa Ubalozi wa Brazil nchini wakibadilishana mawili matatu na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
 Ulifika wakati wa maakuli.
 Mke wa Balozi wa Brazil Mama Luz (Kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa nyumbani kwake Oysterbay wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 189 ya Uhuru wa nchi hiyo.
 Bwana na Bibi Alfonso E. Lenhardt Balozi wa Marekani nchini.
Kwa picha zaidi kuhusiana na ghafla hii Bofya Read More

 Muda vitafunwa ukafika.
 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou akizumgumza mawili matatu na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya maadhimisho ya miaka 189 ya Uhuru wa Brazil yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo nyumbani kwa balozi wa Brazil nchini.
 Mwenyekiti wa mfuko wa Mwl. Nyerere Foundation Bw. Joseph  Butiku (katikati) akibadilishana mawazo katika hafla hiyo.
 Kina mama wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo.
 Afisa Ubalozi (kulia) akiwa na wadau katika hafla hiyo.
Vicheko na furaha vilitawala.

No comments: