
NI wiki nyingine tena tunakutana kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kilasiku kama kawaida.
Mimi kwa kifupi niko poa na wiki hii nitazungumzia hasara tano anazoweza kuzipata mwanaume ambaye anamruhusu mpenzi/mke wake kuvaa nusu uchi kisha kukatiza mtaani. Nalazimika kugusia hili kwa kuwa huko mtaani kuna ‘kijiulimbukeni’ flani ambacho nahisi nikikinyamazia, nitakuwa siwapendi wale wanaofanya hivyo.
Mimi kwa kifupi niko poa na wiki hii nitazungumzia hasara tano anazoweza kuzipata mwanaume ambaye anamruhusu mpenzi/mke wake kuvaa nusu uchi kisha kukatiza mtaani. Nalazimika kugusia hili kwa kuwa huko mtaani kuna ‘kijiulimbukeni’ flani ambacho nahisi nikikinyamazia, nitakuwa siwapendi wale wanaofanya hivyo.
Jamani, sikatai kuwepo kwa uhuru wa mtu kuchagua avae nini anapokwenda wapi lakini kiukweli hili tusipokuwa makini nalo, ipo siku tutajuta na kujiona kuwa hatukuwa tukifanya kitu sahihi.
Wewe ni mke wa mtu, hivi kuna raha gani kukatiza mbele za wanaume ukiwa umevaa nguo ambayo inaonesha kila ulichovaa ndani? Unajisikiaje pale unapopita mtaani ukiwa umeyaanika matiti na mapaja yako?
Kwa jibu la haraka wanaovaa hivyo ni wale wanaojinadi kwa wanaume na wengi ni machangudoa ambao kila walipo wanatega, wanasaka chansi ya kuuza miili yao, sasa na wewe mke wa mtu una nia gani? Unataka kuwaonesha jinsi ulivyoumbika? Haya kama ni hivyo, ili iweje sasa? Wakutongoze?
Mimi huwa napata tabu sana kuwaelewa wanawake wasioijali miili yao na nahisi wanataka kujitengenezea mazingira ya kukinadi kile ambacho kinastahili kuonwa na waume au wapenzi wao tu.
Falsafa ya mapenzi inaeleza kuwa, kuna sehemu za mwanamke ambazo anayestahili kuziona ni mume wake tu, tena wakiwa faragha. Nazungumzia sehemu za kuanzia kwenye magoti hadi kwenye kifua. Lakini mbaya ni kwamba, sehemu hizo siku hizi kila mmoja anaziona kiasi kwamba hata mpenzi wake anapokutana naye haoni jipya.
Achilia mbali hilo, wapo wake za watu ambao wanakatiza mtaani wakiwa wameyaanika makufuli yao kutokana na suruali wanazovaa, hili ni tatizo lakini sasa nilichobaini ni kwamba, wenye matatizo zaidi ni wanaume wanaowaruhusu wapenzi/wake zao kuvaa nguo za ajabu.
Leo nigusie athari zinazoweza kumpata mwanaume ambaye anaona poa mpenzi wake kuvaa nusu utupu kisha kukatiza mbele za wanaume.
Unajishushia heshima
Mwanamke anayetembea nusu uchi hawezi kuheshimika katika jamii na mume/ mpenzi wake ataonekana ‘bogasi’ kwani itachukuliwa yeye ameridhia mali zake kuachwa wazi. Kwa maana hiyo kama unachukulia poa mpenzi wako kuvaa mavazi ya ajabu, unajishushia heshima pia.
Hakuna kizuizi, utasalitiwa tu
Wanaume wakware wanapomuona mwanamke kavaa kimtego wanajua wanatangaziwa biashara hivyo watatatumia gharama yoyote kuhakikisha wanampata. Hivyo basi, kama mkeo ana kasumba ya kutoujali mwili wake na wewe humkaripii, ujue anakusaliti na kama bado basi tarajia hivyo.
Huwezi kulifaidi penzi peke yako
Sehemu nyeti za mwanamke anayestahili kuziona ni mume/mpenzi wake. Mpenzi wako kutembea nusu uchi anakufanya wewe mwenye mali kutoona jipya kwake. Sehemu ambazo ulistahili kuzifaidi peke yako tayari wameshazifaidi wengine kwa macho kama si kwa vitendo.
Mkeo kajazia kisha kavaa nguo laini, ndani hajavaa kitu halafu amepanda kwenye daladala ambalo limejaa na yeye kasimama na kuzingirwa na wanaume, unadhani nini kitatokea? Kama hujui wanaume wengine wanamaliza haja zao katika mazingira hayo, sasa uko tayari mtu ambaye unampenda awaridhishe wengine kingono? Jibu unalo.
Unaonekana humjali, humpendi
Kama kweli unampenda na kumjali mkeo/mpenzi wako, huwezi kumruhusu atoke nyumbani akiwa amevaa kihasara. Kitendo cha wewe kumchukulia poa kwa mavazi yake yasiyo ya heshima inaonesha jinsi usivyomjali wala kumpenda. Yaani ina maana hata akitoka kama alivyozaliwa, huoni hatari.
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.
Chanzo:Global Publishers
No comments:
Post a Comment