Timu ya Tanzania,DC Nyalugusu Sports Club

Timu ya Kenya,Vitambi FC
Timu ya DC Nyalugusu Sports Club timu inayoundwa na vijana,Washington,DC jana Jumamosi iliibanjua bila huruma timu ngumu ya Vitambi FC ya ndugu zetu Wakenya wanaoishi DC.
Mchezo ulikua mkali uliotawaliwa zaidi na DC Nyalugusu,waliokua wakicheza kwa kujiamini na kuonyesha kwamba mchezo uliopita hawakushinda bahati mbaya na pia mwamuzi hakuwa upande wao.
MPAMBANO WA KUKATA NA SHOKA
Leo Jumapili Oct 9,2011 Meadowbrook Park kuna mechi nyingine ya kukata na shoka kati ya Bongo Real FC pia ya DC inayoundwa na wachezaji waliocheza mpira siku nyingi itakayotoana jasho na timu ngumu ya Ubalozi Washington,DC ambayo tangia kuanzishwa kwake haijapoteza mchezo.
Timu kepteni wa Ubalozi Brigedia Jenerali Maganga,amesema wachezaji wake wapo kwenye ari kubwa ya ushindi,timu ya Ubalozi ikiongozwa na Afisa Sulemani Saleh ambae atakua mwiba mkali kwa Bongo Real FC,akisaidiwa na Fowadi machachali Dr Mkama na Afisa Masanja,bila kuwasahau Taji,Eliud Mbowe na Mayor huku wakiongezwa nguvu na vijana wao wenye kukimbia bila kuchoka muda wote wawapo uwanjani watazima ndoto za Bongo Real FC wanaofikiria watapata ushindi mteremuko,Brigedia Jenerali Maganga aliongezea kwa kusema hiki ni kilima cha sekenke mjiandae kukipanda na mvua ya magoli inawasubili.
Timu Kepteni wa Bongo Real FC,Ally Bambino amesema kwao ushindi ni lazima na amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani watapata burudani tosha yakufungia summer,mechi itachezewa ndani ya Park ya Meadowbrook
mechi itaanza saa 10:30(4:30pm) jioni wachezaji wote mnaombwa mfike 10:00 kamili jioni(4:00pm)
WOTE MNAKARIBISHWA

Timu ya Ubalozi
Timu ya Bongo Real FC

No comments:
Post a Comment