Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Harith Juma Mwapachu wakati wa maziko yake kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Harithi ni mtoto wa Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, alikufa Jumanne, Dar es Salaam. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal.(Picha na Freddy Maro). |
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL), Bi. Teddy Mapunda akimkabidhi Kamnda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Bw.Mohamed Mpinga moja ya nakala ya vitabu 20,000 vya elimu ya usalama barabarani vitakavyotolewa bure kwa madereva na watu mbalimbali ili wawe na uelewa wa namna ya kuepuka na ajali zisizo za lazima. Shughuli ilifanyika Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. John Tupa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la Idara ya Habari kuhusiana na maandalizi ya Mbio za Mwenge wa uhuru unaotarajia kuwashwa mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga, Kaimu Ofisa Utamaduni na Michezo, Bw. Shekheadi Saidi (kushoto). Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Clement Lujaji (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Karaine Kimaati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Hawa Ghasia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na 12 ya kifo cha Muasisi wa Taifa la Tanzania, Mw. Julius Nyerere yatakayofanyika Dar es Salaam kesho kutwa.
No comments:
Post a Comment