Korea Kusini imeipatia Tanzania mkopo wa Sh. bilioni 103.6 kusaidia upanuzi wa vituo vinne vya umeme na vifaa tiba.
Mkopo huo umetolewa na Benki ya Exim Korea, kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi (EDCF).
Hafla ya kutia saini ilihudhuriwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, wambaye aliishukuru serikali ya Korea kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali.
Waziri Mkulo alisema sehemu ya fedha hizo itatumika kupanua mradi wa umeme katika mikoa ya Iringa, Shinyanga, Dodoma na Singida na uwekaji wa vifaa tiba utafanyika katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS) kampasi mpya ya Mlonganzila, Kwembe.
Alieleza kuwa Sh.bilioni 59.9 zitatumika kwa ajili ya kupanua mradi wa umeme Iringa-Shinyanga na kwa ajili ya mkondo wa kusafirisha umeme wa KV 400. Mradi huo utasaidia maeneo ya wa kusini na mashariki ya Tanzania.
Aidha, alisema mkopo wa pili ni wa Sh. bilioni 44.1 utatumika katika maendeleo ya MUHAS ambao utahusisha usambazaji wa vifaa vya tiba na uwekaji wa vifaa hivyo.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment