Timu ya Tanzania,DC Nyalugusu Sports Club

Timu ya Kenya,Vitambi FC
Kesho Jumamosi asiye kuwa na mwana aeleke jiwe ni mpambano wa kukata na shoka wa marudiano kati ya Timu yetu ya Tanzania,DC Nyalugusu Sports Club ambayo itashuka dimbani kupepetana na jirani zetu kutoka Kenya wanaoishi DC,Vitambi FC.
Mechi inatarajiwa kua kali kwani mechi ya kwanza timu hizi zilipokutana zilitoka sare ya goli 2-2 kwenye mpambano uliokua wa vuta ni kuvute.
Kocha wa DC Nyalugusu Jabir Jongo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi,mechi itaanza saa 10:30 jioni(4:30pm) uwanja wa Beach Drive unaopakana na Meadowbrook park. ilikochezewa mechi ya Vijana na Wazee.
Jumapili kutakuwa na mechi nyingine kati ya Timu ya Ubalozi,Wshington,DC na timu ya Bongo Real mechi itategemewa kuwa ngumu kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kua na uzoefu wa muda mrefu wa kusukuma gozi la ng'ombe.
Kocha mchezaji wa Bongo Real FC,Ally Bambino amesema wachezaji wake wapo kwenye hali nzuri kimchezo na mashabiki wa Bongo Real wategemee ushindi mnono.
Timu kepteni wa Ubalozi Brigedia Maganga amesema mdomo hauchezi mpira vijana wetu wakishirikiana na Wazee wao wataonyesha soka la kitabu ole wenu Bongo Real kukubali kucheza mechi hii,sisi ndio Ubalozi timu inayosakata kabumbu ya uhakika na mashabiki mfike kwa wingi kwani hii itakua zawadi tosha ya kumalizia summer
Mechi itachezewa Meadowbrook park
7901 Meadowbrook LN
Chevy Chase,MD 20815
Mtanange utaanza 4:30 pm

WOTE MNAKARIBISHWA
No comments:
Post a Comment