
NI mjadala mrefu hakika, ambao unaweza kujadiliwa karne kwa karne lakini jibu la moja kwa moja lisipatikane. Hapa kila mmoja atasimamia kile anachokiamini zaidi. Inawezekana nikasema wanawake wa kijijini ni bora zaidi na wafaa kuwa wake bora, lakini yupo aliyetendwa na mwanamke wa namna hiyo.
Pengine umewahi kusikia kwamba, ukioa mwanamke wa mjini ni vyema maana anakuwa ameshaujua mji na mabaya yake, hivyo si rahisi kukusumbua, kumbe tayari ipo mifano ya waliolizwa na wanawake wa namna hiyo.
Pengine umewahi kusikia kwamba, ukioa mwanamke wa mjini ni vyema maana anakuwa ameshaujua mji na mabaya yake, hivyo si rahisi kukusumbua, kumbe tayari ipo mifano ya waliolizwa na wanawake wa namna hiyo.
Ndoa ni suala zito ambalo linahitaji utayari zaidi wa wahusika na pendo la kweli. Ukiachana na hilo kuna suala la hulka, tabia na haiba. Unaweza kumdhania ndiye, kumbe siye. Utulivu huhitajika katika kung’amua hili.
Bila shaka rafiki zangu mpo wazima wa afya njema, tayari kupokea kile nilichowaandalia. Msishangae nimechelewa kuwasabahi, ni kutokana na haraka ya kutaka kuanza mada ya leo. Hebu twende tukaone.
WANAWAKE WA KIJIJINI
Je, ni kweli kwamba mwanamke wa kijijini ni bora zaidi kuliko wa mjini? Wapo wanaofikiria hivyo, lakini hapa nitakupa faida na hasara za wanawake wa kijijini, ambazo zitakupa mwanga wa uchaguzi wa mke bora.
FAIDA
Haya ni baadhi ya mambo mazuri ambayo mwanamke wa kijijini anakuwa nayo. Mwanamke huyu anaelezwa kuwa na heshima kupindukia, siyo mkaidi, muelewa na mwenye heshima sana kwa mumewe.
Hana makuu, hapendi starehe, anajali familia yake, ndugu wa mumewe na hata marafiki wa karibu wa mume wake. Anajua shughuli za nyumbani kama mke, lakini pia ni mtafutaji mzuri kwani mara zote hujishughulisha na biashara ndogo ndogo au kilimo.
Ni mwepesi kuelewa mambo, hasa kama anakatazwa au kuonywa. Anajua nafasi yake kama mke na ‘anacheza’ ipasavyo katika nafasi hiyo. Anaweza kuishi maisha ya aina yoyote.
HASARA
Inaelezwa kwamba, asilimia kubwa ya wanawake wa vijijini hawajaenda shule! Wengi huishia darasa la saba na kuolewa au kubaki nyumbani. Hili huvumbua kasoro nyingi nyuma yao, lakini kubwa zaidi wanakuwa hawana ufahamu wa mambo mengi.
Hawajui dunia inaendaje, mawazo yao siyo endelevu na siyo mapana. Hawana mipango ya muda mrefu, wanategemea zaidi mume kwa kila kitu. Baadhi yao huamini kuolewa ndiyo kila kitu na mume ndiyo kila kitu katika nyumba na maisha kwa ujumla.
Kwamba anaweza kufanyiwa kila kitu na mumewe kwa sababu eti ni mume! Siyo mwepesi wa kugundua makosa au matatizo haraka. Ni rahisi kufanya jambo baya na kung’amua baadaye sana ubaya wa jambo alilolifanya.
Siyo mjanja, ni mzito kifikra. Muoga kujifunza. Baadhi yao hupelekwa unyagoni ambapo hufundwa na kuelekezwa anayotakiwa kuyafanya kama mwanamke. Mara nyingi hupelekwa huko akiwa na umri wa kuanzia miaka 13-15, akitoka huko anaamini tayari yeye ni mtu mzima!
Anaanza kufanyia mazoezi aliyofundishwa! Mafunzo yanayotolewa huko yanadaiwa kuwa si mazuri sana, kwani mtoto hufundwa mambo mazito ambayo anapaswa kufundwa mwanamke ambaye anajiandaa kuingia kwenye ndoa. Kuharibikiwa huku mapema, wakati mwingine kunaweza kumuathiri hata anapokuwa mtu mzima na familia yake.
MWANAMKE WA MJINI
Kama tulivyoona kwa wanawake wa vijijini, wa mijini nao wana mazuri na mabaya yao. Tazama vijipengele hivi hapa chini, ambavyo vinachambua baadhi ya mazuri na mabaya yao.
FAIDA
Wengi ni wajanja wa kila kitu, uelewa, akili na hata utafutaji. Wengi wameelimika (angalau wamefika kidato cha nne na kuendelea). Ambao wamesoma vyuo mbalimbali wana nafasi kubwa ya kuajiriwa katika makampuni mbalimbali jambo linaloweza kuweka mgawanyo wa kutimiza majukumu ndani ya nyumba.
Mwanamke huyu ana msimamo, siyo rahisi kuyumbishwa, anatumia akili zaidi kuliko nguvu. Hana papara na mambo yake, hupangilia pointi zake katika kumkosoa mwanaume. Mchakarikaji, mchangamfu, anajua mahaba, akili yake imepanuliwa na utandawazi wa ukuaji wa Sayansi na Teknolojia.
Siyo ‘mshamba’, anajua kila kitu, siyo mgeni sana na wanaume (hasa matapeli), ni muwazi, mwepesi kushauri/kushauriwa na liwazo la kweli mwenzi wake anapokuwa mgonjwa.
Mwanamke huyu haogopi kukushauri unapokwama (hata kama hujamwomba afanye hivyo). Pia baadhi yao wanapenda kujiendeleza kielimu jambo ambalo linazidi kuwapa nafasi ya kuwa wake bora zaidi. Hoja hujibiwa kwa hoja.
Hutumia vitu vya kisasa kuhakikisha penzi linazidi kuwa imara. Anatambua haki zake kama mwanamke, lakini pia anajua wajibu wake kwa mumewe.
Wiki ijayo tutaona hasara zao, kabla ya kuhitimisha mada yenyewe. Unadhani mwanamke yupi ni bora? Kijijini au mjini? Wiki ijayo utapata majibu, USIKOSE!
Joseph Shaluwa ni mshauri wa mambo ya mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Secret Love vilivyopo mitaani.
4 comments:
mwanamke bora hupatikana kwa mungu. vilevile kila mtu ana choice yake, wapo wanaotaka wanawake wa kukaa home, so wa vijijini wanawafaa. wapo wanaopendelea career women wanaonukia manukato 24/7, wa mjini ndo size yao
mwanamke bora mjini,kijijini kuna raha yake lakini ukimleta mjini akishaujua mji baraa ndio hapo linapohanza
"Mke mzuri ni kutoka Tanzania au wa hukuhuku majuu ?"
Nyumba na mali,mtu hurithi kwa baba yake,
Bali MUME/MKE mwenye tabia njema mtu hupewa na MUNGU.
Mithali.
jaribu kuleta mke kutoka bongo uone jeuri yake!
Post a Comment