ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 19, 2011

Sherehe kufuatia kubadilishana wafungwa-BBC

Ghilad Shalit akikariobishwa na babake, Waziri Mkuu Netanyamu na, waziri wa ulinzi Ehud Barak
Makundi ya watu wenye furaha nchini Israel na Palestina wamekuwa wakisheherekea mpango wa kihistoria wa kubadilishana wafungwa.
Israel iliwaachiliwa huru mamia ya wafungwa wa Kipalestina, ikiruhusu wengi wao kurudi katika eneo la Gaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, na badala yake kukabidhiwa askari wa Kiisrael Gilad Shalit.
Sajini Shalit aliyekuwa amezuiliwa katika eneo la Gaza kwa zaidi ya miaka mitano, alipokelewa kishujaa alipowasili nyumbani kwake.

Shalit mwenye umri wa miaka 25, hatimaye alilala nyumbani kwao na familia yake kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa huru.
Babake Shalit amesema mwanawe ana matatizo ya kutangamana na watu kutokana na kuzuiliwa kifungo cha upweke cha miaka mingi, kwa hivyo hangeweza kuhutubia waliojitokeza kumkaribisha.
Alisema anaeleewa machungu yanayozikumba familia ambazo zimepoteza wapendwa wao waliouawa na Wapalestina walioachiliwa huru wakati wa kubadilishana wafungwa.

mpango wasifiwa

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wa viongozi wa kundi la kiislamu la Hamas walioafikiana kuhusu kubadilishanaji kwa wafungwa hao, walisifu hatua hiyo kama thibitisho la sera zao.
Lakini waandishi wa habari wamesema kubadilishana kwa wafungwa huenda kusiwe na athari kubwa katika mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.
Wakati hayo yakijiri, zaidi ya watu laki moja walijumuika katika ukumbi maalum mjini Gaza kusherehekea kuachiliwa huru kwa nusu ya zaidi ya Wapalestina 1000.
Mji wa gaza uko chini ya kundi la Hamas na kiongozi wa kundi hilo Khaled Meshal alisema limepata ushindi mkubwa kufuatia hatua hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

sherehe hii ina pande mbili