ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 14, 2011

Suluhu haipatikani nje ya ndoa

NAAM kama ilivyo ada tumekutana tena washirika ili kujua mtumishi wenu nimewaletea nini. Nimepata maswali mengi juu ya matatizo ndani ya ndoa au kwenye uhusiano wa kawaida wa kimapenzi. Imeonyesha pande zote zinafikisha lawama zao huku zikiwa tayari zimeshatafuta tiba mbadala kabla ya swali.

Ni matatizo gani hayo?
Moja ni kukosekana kwa uaminifu kwenye ndoa, pili kushindwa kupatiwa penzi kamili. Katika maswali haya, mmoja alidiriki kusema kuwa licha ya bwana wake kuwa naye mbali bado amekuwa hakidhi haja zake, hali inayomfanya awe kwenye mateso kila siku chache anazokuwa yupo nyumbani.


Fikra zake zikamsababisha kutaka kutafuta mtu wa pembeni ili awe anamsaidia mume wake anapokuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka miwili.

Kwa upande wake aliona ule ndiyo utatuzi wa tatizo lake, lakini uamuzi huo ulikuwa mgumu na ndipo akaamua kuomba ushauri kabla ya kufanya hicho alichokiwaza.

Kama ilivyo ada kwa uwezo mdogo niliopewa na Muumba, nilimshauri na kunielewa. Baada ya kumjibu niliamini wapo wengi wenye matatizo kama hayo na wamekuwa wakifa na tai shingoni au kutoka nje ya ndoa zao kutafuta suluhu.
Nageukia kwako mwenye wazo kama hilo, unapokuwa mwepesi wa kutoa uamuzi bila kuangalia hasara ni hatari.

Unapotokewa na tatizo la mwenzio kushindwa kukufikisha au mpenzi wako kuwa mtu wa kusafiri, kwanza napenda kukuomba uwe mvumilivu na kulilinda penzi lako, najua unakuwa kwenye hali mbaya, lakini hiyo si sababu ya kutoka nje ya ndoa.

Siku zote unapokuwa kwenye wakati huo, jiepushe na mawazo ya ngono au kuangalia picha za ngono ambazo zitakupa kishawishi cha mapenzi.
Siku zote mawazo ya mtu huelekea unapoyaelekeza, pia moyo una haki ya kutamani lakini wewe ndiye unayetakiwa kuuzuia, kama ukiendekeza utakupeleka kubaya.

Kuwa muwazi
Unatakiwa kuwa mkweli kwa mpenzi wako, kumueleza unavyoteseka ili mtafute utatuzi. Huenda yeye huamini wewe hufurahia kumbe sivyo.

Hata wewe mwanaume lazima umsome mpenzi kwa kuelewa muda gani anafurahia kile unachompa hata bila kusema. Raha ya safari katika mapenzi ni kufika kilele, kama mwenzako humfikishi lazima utajua hujamkidhi haja hivyo jitahidi na yeye afike.

Katika ndoa hakuna kitu mwanamke alichokifuata kwako zaidi ya mijeledi. Nani alikuambia punda au farasi anakufa kwa mijeledi. Kupigwa kwake ndiko kunakomfanya aongeze mbio.

Katika mapenzi, mijeledi huongeza upendo hata kuondoa mawazo mabaya kwa mkeo kukusaliti. Pamoja na kufanya kazi nzito ambazo huchosha mwili, unatakiwa upate muda wa kumpanda punda wako na kumpiga mijeledi ambayo hautakiwi kumuhurumia kwani kwake kipigo hicho ndiyo raha yake.   

Kuweni wawazi na wakweli ili kuwekana wazi kila mmoja ajue kitu gani mwenzie amepunjwa hasa katika mapenzi. Ili kumnyima nafasi shetani ambaye kishawishi chake kikubwa ni wewe kutoka nje ya ndoa.
Namalizia kwa kusema hakuna suluhu ya matatizo nje ya ndoa yako zaidi ya kujidhalilisha kwani penzi la kweli limo ndani ya ndoa, nje ya hapo ni kupotea njia.

Kama una wazo la kuisaliti ndoa yako jiulize mara 10 faida na hasara zake. Ikiwa kuna tatizo kaeni chini na mwenzako mtafute suluhu ambayo ndiyo kinga thabiti ya ndoa yenu.

Kwa hayo machache tukutane wiki ijayo.

www.globalpublishers.info

No comments: