ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 8, 2011

VIDA MAHIMBO NEW LINE SASA KUPATIKANA FUCHSIA @ GOLDEN TULIP HOTEL

Mbunifu maarufu wa mavazi kitaifa na  kimataifa Vida Mahimbo leo amezindua rasmi nguo za VIDA MAHIMBO NEW LINE FOR "CURVY WOMEN" anazoziuza katika duka la nguo la Fuchsia Boutique lililopo katika hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam pamoja na duka lake la Slipway Shopping Centre-VIDA MAHIMBO STORE.
 Vida Mahimbo katika picha ya pamoja na familia yake. Kushoto ni Mama yake Bi. Edna Mahimbo, Dada yake Sophia pamoja na mtoto Abigael.
Baadhi ya wateja wakiangalia nguo na kupata ushauri kutoka kwa Mbunifu wa Mavazi nchini Vida Mahimbo(katikati). 
 Mtaalamu wa Masuala ya Urembo na Make Up Jackie Hamilton (kushoto) akifafanua jambo kwa wateja waliotembelea duka hilo.
 Muonekano wa nje wa Duka la FUCHSIA BOUTIQUE lililopo Golden Tulip Hotel.
 Wateja kutoka mataifa mbalimbali wakishangaa ubunifu wa Vida Mahimbo.
 Mmoja wa Wateja akishine na Ubunifu wa Vida Mahimbo.
 Huu ni size yako kabisa.
 Wateja kutoka mataifa mbalimbali wakishangaa ubunifu 
 Mmiliki wa FUCHSIA BOUTIQUE Duka linalouza NEW LINE ya Vida Mahimbo Alka Chande (kulia) akionyesha wateja mitindo ya nguo alizozibuni. Alka ni mshirika wa karibu wa Vida Mahimbo.
 Vida Mahimbo  akitoa huduma kwa wateja wake
 Vida Mahimbo akielezea Ubora wa Nguo za Line ya Uhuru kwa wageni kutoka Marekani ambao wamevutiwa na kazi zake.
  Mdau wa Masuala ya Fashion na Mavazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Karshima Fashion Group Ltd. Ayesha Samji sambamba na wateja wa Nguo za Vida Mahimbo.
Mmoja wa wateja katika vazi la Khanga lililobuniwa na Vida Mahimbo.
(Picha kwa hisani ya www.mohammeddewji.com/blog)

No comments: