Saturday, November 12, 2011

AMANI NA UTULIVU WAREJEA GHAFLA MKOANI MBEYA NA SHUGHULI KUENDELEA KAMA KAWAIDA KUANZIA LEO, MMTU MMOJA AFARIKI KATIKA VURUGU ZA SIKU MBILI

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama katika jengo la kitega uchumi la OTTU lililopo stendi ya magari madogo ya abiria(daladala), mara baada ya Mbunge Mbilinyi kuhutubia wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama mwenye shati la miraba ya samawati(Katikati) katika picha ya pamoja kabla ya Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi  Kuhutubia.
Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila kupora bidhaa madukani.
 Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Maelfu ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
 Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), likiwasaidia Jeshi la Polisi kuweka hali ya amani na utulivu mara baada ya kuisha kwa mkutano uliofanyika katika kituo cha mabasi madogo ya abiria(daladala) eneo la Kabwe Mwanjelwa jijini Mbeya
Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa sikumbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi.
NB:- Mtu mmoja afariki, watano wajeruhiwa kwa risasi na 235 wakamatwa, Mbunge ataka waachiwe bila Masharti yoyote.

Habari na picha na Mbeya Yetu Blog

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake