Hapa akimkabidhi fedha bi Hawa Abdallah,ambaye ni mama mzazi wa marehemu Mbwana Masoud
Mama akilia kwa uchungu baada ya kukumbuka msiba wa mwanaye baada ya kukabidhiwa fedha za rambirambi
Ndg.Wilfred Lwakatare akitoa maneno ya kufariji familia ya Mbwana muda mfupi kabla ya kutoa rambirambi
Mzee Yusuph Rule, akiongea kwa niaba ya familia ya wafiwa.
--
Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa kagera, kimetoa shilingi laki tatu na themanini na nne elfu(384,000/=) kwa familia ya marehemu Masoud Mbwana,mwanachama wa chama hicho anayedaiwa kuuawa igunga kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge ambapo alikwenda kuwa wakala wa chama chake.Rambi rambi hiyo imewasilishwa leo Mburahati mtaa wa makurumla kwa Jongo jijini Dar es salaam,nyumbani kwa marehemu.
Aliyewasilisha ubani huo ni ndg W. Lwakatare mwenyekiti wa mkoa wa Kagera kwa niaba ya viongozi,wanachama wa Chadema Kagera na wananchi wa mkoa huo.Fedha hizo zimechangwa na viongozi wa chama hicho waliokuwa na kikao cha kawaida walipopata taarifa za msiba wa mbwana.Mh.Lwakatare ameomba jamii kuendelea kujali ndugu wanaofikwa na matatizo.Aliambata pia na katibu mwenezi wa jimbo la Ubungo ndg Ali Makwilo na katibu wa chama Ubungo ndg Nassoro Balozi.
Chanzo:24 SEVEN 365
No comments:
Post a Comment