Wageni waalikwa kutoka taasisi na balozi mbalimbali wakiwa katika ukumbi wa Mlimani City kushuhudia Mkutano Mkuu wa Chama Taifa leo tarehe 21 Januari 2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) FREEMAN Mbowe amewasihi viongozi watakaoshika nyazifa mbalimbali katika Chama hicho ni lazima wakijenge chama katika misingi ya maadili na Nidhamu.
Ameyasema hayo leo Januari 21, 2025 wakati anafungua Mkutano Mkuu wa chama hicho unapendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam.
"Mtakaopewa mikoba ya chama hiki ni lazima mkarekebishe, inawezekana tukavumilia matusi kipindi hiki cha chaguzi lakini msingi wa Chadema sio matusi watakaokabidhiwa mikoba leo wakasafishe"
"Hiki chama tunawajibu wote wa kukilinda kwa gharama yoyote ile na chama hiki tutakilinda". Ameongeza.
Amesema kuwa Chadema kitamaliza uchaguzi wakiwa wamoja na kwamba uchaguzi huo sio vita.
No comments:
Post a Comment