Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni za GURJAR GRAVURES na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED za nchini India Bw. Zainuddin Mahuwala (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) hundi ya $ 15,000/= kwa ajili ya kusaidia jitihada zake za kuboresha Maendeleo katika jimbo lake la Singida Mjini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hizo Bw. Shubair Mahuwala.
Bw. Zainuddin Mahuwala pamoja na Mwanae Shubair Mahuwala wakimfafanulia Mh. Mbunge kuwa fedha hizo zimetolewa na kampuni zao mbili ambapo kila moja imetoa kiasi cha $ 7,500/=.
Mh. Mohammed Dewji akionyesha karatasi zenye hundi aliyokabidhiwa leo ofisini kwake.
Mh.Mohammed Dewji katika picha ya kumbukumbu na ugeni wake uliomuunga mkono kwa kumkabidhi hundi ya $ 15,000/=.
Na.Mwandishi wetu.
Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji leo amepokea jumla ya dola za kimarekani elfu 15 kutoka kwa kampuni ya GURJAR ya India kutokana na mchango wake katika kutoa huduma kwa jamii hususan kuwasaidia yatima na watoto ambao wazazi wao hawana uwezo.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa na kampuni mbili zinazomilikiwa na Zainuddin R. Mahuwala za GURJAR GRAVURES PRIVATE LIMITED ambayo imetoa dola 7,500 na GURJAR IMAGES PRIVATE LIMITED ambayo imetoa dola 7,500.
Akipokea hundi ya fedha hizo Mh. Dewji amesema atazielekeza katika mfuko wa huduma za elimu wa Mohammed Foundation ambao umekuwa ukisaidia kuwasomesha watoto zaidi ya 2400 katika jimbo la Singida Mjini.
Wakati wa makabidhiano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ofisini kwa Mh. Dewji, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hizo Bw. Zainuddin Mahuwala ambaye aliambatana na mtoto wake Shubair Z. Mahuwala ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hizo, amempongeza sana mbunge huyo na kumtaka kuendelea na moyo huo wa kusaidia jamii huku akimuombea Mungu amzidishie.
Mh. Dewji amekuwa akipigania kupatikana kwa fursa sawa ya elimu kwa watoto Singida mjini ikiwemo kujitolea kukarabati na kujenga shule sambamba na kununua vifaa vya elimu. Kwa sasa Mh. Dewji anasomesha watoto zaidi ya 2400 yatima na ambao wazazi wao hawana uwezo ili nao wapate nafasi ya kupata elimu itakayowasaidia kujikomboa katika maisha.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake