WIKI iliyopita nilitoa mfano wa Ester na Sam. Jinsi ugomvi wao ulivyochukua nafasi kubwa hata baada ya kuachana kiasi cha kusababisha hata wasiohusika wajue.
Kimsingi mada hii ina lengo la kukutaka uwe wa kwanza kulinda heshima yako. Usipojiheshimu wewe hakuna hata mtu mmoja atakayekuheshimu. Usipojidhibiti, mapenzi yanaweza kukupa ugonjwa.
Sizungumzii magonjwa yanayotibika hospitali au kwa Babu Loliondo, namaanisha maradhi ya kukosa utulivu wa kichwa na moyo. Lazima uwe wa kwanza kuhakikisha huugui ‘umapepe wa mapenzi’.
Kimsingi mada hii ina lengo la kukutaka uwe wa kwanza kulinda heshima yako. Usipojiheshimu wewe hakuna hata mtu mmoja atakayekuheshimu. Usipojidhibiti, mapenzi yanaweza kukupa ugonjwa.
Sizungumzii magonjwa yanayotibika hospitali au kwa Babu Loliondo, namaanisha maradhi ya kukosa utulivu wa kichwa na moyo. Lazima uwe wa kwanza kuhakikisha huugui ‘umapepe wa mapenzi’.
Kila mtu anapenda kwa maana ya yule ambaye nafsi yake imemdondokea. Lakini haijawahi kusemwa kwamba mapenzi ni utumwa.
Inawezekana ukawa hujapata mantiki ya hoja yangu hapo. Labda nikufafanulie kuwa tatizo linalowakabili watu wengi ni kushindwa kusoma alama za nyakati.
Namaanisha kutokufahamu kipimo cha mapenzi na wakati wake. Inawezekana alikupenda na unampenda lakini mabadiliko yake yakupe picha ili ujue cha kufanya.
Unangoja akuoneshe mpenzi mwingine ndiyo ujue kuwa zama zako zimefika tamati? Akufukuze kama mbwa na matusi juu? Usingoje aibu, heri nusu shari kuliko shari kamili.
Thamani yako ni kubwa mara sabini kama utakuwa mwelewa na kujiondoa kuliko taadhira ya kutupiwa virago. Kuna penzi hai na lililokufa, weka akilini na uheshimu.
Nilishafafanua mambo mengi kuhusiana na jinsi ya kulikabili penzi lililokufa, njia moja ambayo niliisisitiza ni kuinua mikono. Kulazimisha mapenzi ni gharama kubwa ambayo si rahisi kuifidia.
Hata hivyo, ni vema nikupe mbinu za awali. Hapa sitoi ushauri wa aina moja. Natoa njia nyingi ili uchague ya kushika kabla ya kupata suluhu.
Hapa chini kuna mambo ya msingi ya kufanya pale unapoona mwenzi wako amebadilika. Ukishindwa yote hayo, hapo hutakuwa na la kufanya zaidi ya kuinua mikono. Uking’ang’ania, ni sawa na kukumbatia penzi lililokufa. Utateseka, utaaibika.
1. MSIKILIZE
Mpenzi wako anapokasirika na kukujia juu, unatakiwa umsikilize kwa makini. Mpe nafasi ya kuzungumza hata kama unahisi anakuonea.
Kwa kufanya hivyo ataona umemheshimu na kumjali, hasira zake zitapungua. Katika utulivu na usikivu, suluhu ya kweli hupatikana.
2. JIDHIBITI
Mwenzi wako anapopanda juu kwa hasira na ghadhabu, hupaswi kuoneshana naye ubavu. Jifanye mjinga na dhibiti hisia zako, atatulia.
Kujaribu kubishana kutafanya tatizo liwe kubwa zaidi. Hata kama anatoa maneno ya kukasirisha, jidhibiti kuepusha shari zaidi.
3. MKUBALIE ANACHOKITAKA
Unapoonesha kiburi au dharau kwa mpenzi wako anapokuwa amekasirika, tambua kwamba unaongeza ukubwa wa tatizo.
Kama anakung’ang’aniza kukubali jambo ili aibuke mshindi, mkubalie ili mfikie muafaka. Hata kama unaona anachokulazimisha siyo sahihi, kubali kwa wakati huo, hasira zake zikitulia utazungumza naye vizuri.
4. CHUNGUZA KINACHOMKASIRISHA
Wapenzi wengi hulalamika kuwa wenzi wao hurudi majumbani wakiwa tayari na hasira. Hivyo kunapotokea jambo dogo ambalo huenda ni la kawaida, huhamisha hasira zao. Mchunguze mwenzi wako kugundua kinachomfanya akasirike.
Kama hukwazika anapokuwa kazini, akirudi jitahidi kumpa muda wa kutuliza akili na mfariji kwa maneno mazuri, hasira zake zitaisha. Kama hukasirika na uchafu wa mahali mnapoishi, jitahidi kuwa msafi na atazidi kukupenda.
5. USICHOCHEE MOTO
Unapoona mwenzio amekasirika, tambua kuwa moto wa hisia za kuumiza unamuwakia. Ni kosa kuendelea kumletea masihara katika wakati kama huu au kufanya makosa yatakayozidisha hasira zake.
Jitahidi kumhudumia kama mtoto mdogo anapolia. Mbembeleze kwa maneno na vitendo, atarudi kwenye hali ya kawaida. Epuka kauli kama ‘jambo dogo tu linakuudhi?’ Au ‘unakasirika hata bila sababu’.
6. USILALAMIKE
Hata kama unaona mwenzi wako anakutuhumu kwa jambo ambalo hujafanya au lisilo la kweli, hutakiwi kuanza kumlalamikia kuwa anakuonea.
Tulia na mwache hasira zake zitulie. Baadaye utakapoona ametulia na kurudi kwenye hali yake ya kawaida, zungumza naye kwa upole na mweleze yale yaliyo moyoni mwako. Lawama huchochea zaidi hasira.
7. KUBALI MAKOSA
Kama umegundua kuwa wewe ndiyo chanzo cha mwenzi wako kukasirika, kubali makosa na mwonyeshe kwamba unajuta kwa uliyoyafanya. Hutapungua chochote endapo utakiri makosa. Kukiri ni alama ya ukomavu wa hisia, mwenzi wako atakuheshimu.
8. MTAZAME USONI
Wataalamu wa saikolojia za mapenzi wanaeleza kuwa kutazamana usoni (hasa machoni) huwaweka jirani kihisia wapendanao. Kama mwenzio amekasirika sana, mtazame usoni kwa uso angavu usio na hata chembe ya hasira wala kinyongo. Mtazame kwa makini na mwonyeshe kwamba unamsikiliza kwa makini. Hii itakusaidia kuziteka hisia zake na kubadilisha hisia chungu alizonazo kuwa hisia za kimahaba.
9. JIAMINI
Tuliza hisia zako na jiamini kwamba japokuwa mwenzio amekasirika una nafasi ya kumfurahisha na kumfanya asahau yote yaliyomuudhi. Amini kwamba hasira ni sehemu ya maisha na kwamba kila mtu hukasirika.
10. MTULIZE KWA MAHABA
Tendo la ndoa linaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuwafanya wapendanao kubadilishana hisia. Ikiwa mwenzio amekuudhi, hiyo siyo sababu ya kukufanya umbanie haki yake.
Baada ya hasira kutulia, mtulize kwa kumpa mahaba mazito, hii itawaunganisha upya na kuwafanya nyote msahau yaliyotokea na kuanza ukurasa mpya.
ANGALIZO
Kwa nini uambiwe “toka”, “sikutaki” na mengine yenye kukuaibisha na kutesa moyo wako? Unapaswa kusoma alama. Ujue kipimo cha mapenzi yenu ili uwe na pakushikia.
www.globalpublishers.info
1 comment:
Hapo hujasema kabisaa. Kama Mwanaume wako anapumua kwa roho anatakiwa ajue kuwa nawewe Mpenzi wake wa Kike unapumua kwa roho kama yake. Hutakiwi kuwa Mtumwa kwa Mpenzi wako, Mapenzi ni kuelewana ndugu, yawe ya Pande zote Mbili siyo yatoke Pande moja tu kwa Mwanamke. Mwanaume hata umpigie Magoti kiasi gani akishapata mwingine anasahau mlikotoka na kuanza kukuletea Visa vya kila siku, kisa cha kujiua na mtu anakutafutia visa kila siku? Wakati Mwanaume ni Bwana Yesu Peke Yake!! Ukimjali, Ukimtumainia, Ukimheshimu nae Atakurudishia Mara Dufu. Lakini siyo Wanaume wa Ulimwengu Huuu!!
Post a Comment