Sunday, November 6, 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL NA RAIS MSTAAFU WA COMORO WASHIRIKI BARAZA LA IDD NA SWALA YA ID KITAIFA MSIKITI WA AL FAROUK JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakati akipokelewa alipowasili katika viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akimpokea Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad  Abdallah Sambi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba  na Baraza la Idd. 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akipokelewa na mmoja wa waumini wa dini ya Kiislam, Asha Baraka, wakati alipowasili alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na  Baraza la Idd

(picha kwa hisani ya 24 seven 365 Blog)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake