Sunday, November 6, 2011

Prince Charles kuanza ziara nchini kesho

Mtoto wa Malikia wa Uingereza, Prince Charles na mkewe Camilla anatarajia kuanza ziara yake ya siku tatu kesho ya kutembelea miradi mbalimbali hapa nchini mara baada ya kuwasili leo katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Siasa, Habari na Miradi kutoka Ubalozi wa Uingereza hapa nchini, Mark Polatajko, alisema kuwa mtoto huyo wa Mfalme pamoja na mkewe wataanza ziara yao rasmi Jumatatu ambapo pamoja na mambo mengine watafanya mazungumzo na Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Alisema watazungumzia mahusiano kati ya nchi hizo mbili katika masuala ya mawasiliano, sayansi na teknolojia na kuzihusisha wizara mbalimbali katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.

Polatajko alisema kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam, ugeni huo utatembelea maeneo tofauti ikiwemo Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ili kuangalia zaidi juu ya misaada ya kielimu kwa wasichana.
Pia alisema ugeni huo utapata fursa ya kuzitembelea asasi zisizizo za kiserikali zinazojihusisha na masuala ya ubunifu na kampuni endelevu.
Kadhalika alisema watapata fursa za kutambua kazi zilizofanywa katika maafa ya kuzama kwa meli ya MV Spice iliyotokea mwezi Septemba mwaka huu ambayo ilisababisha vifo vya wananchi zaidi ya 3000.
Polatajko alisema siku ya Jumanne ugeni huo utaenda visiwani Zanzibar na watafanya mazungumzo na Rais Dk. Ali Mohamed Chein na maeneo yake ya kitalii na kesho yake utaelekea mjini Arusha na kutembelea Boma la Kimasai lililopo kijijini cha Majengo.
Pia mjini Arusha watatembelea shule ya Legunga kwa ajili ya kujua mahusiano kati ya serikali na wafadhili kwenye kuimarisha upatikanaji wa elimu.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

  1. CORRECTION!!! Charles soi mtoto wa mfamle.ni mtoto wa malkia Elizabeth II wa uingeraza. uk Does not have a King.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake