![]() | |
|
MCHANGO wa Mwalimu Julius Nyerere katika kupigania Uhuru wa Tanzania Bara ni mkubwa.
Katika makala haya, MWANDISHI WETU, MAGNUS MAHENGE amefanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku kuhusu miaka 50 Uhuru iliyopita.
Yafutayo ni mahojiano yenyewe:
Swali: Kama mtu wa karibu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere tangu 1965 ukiwa Ikulu, unajua ni mbinu gani alizitumia kuwahamasisha, kuwaunganisha na kuwashirikisha Watanganyika katika kampeni za kuanzisha Tanu na kudai Uhuru?
Jibu: Mwalimu Nyerere aliwahamasisha Watanganyika na baadaye Watanzania kwa ujumla wao kwanza, wajitambue kuwa ni watu huru.
Nyerere alikuwa kwenye TANU kwa miaka saba hadi nchi inapata Uhuru Desemba 9, 1961 ambapo katika kipindi chote aliwajenga wananchi wajue kuwa wanatakiwa kuwa watu huru na hivyo ni budi wapate uhuru na ndipo watapata maendeleo ya kweli.
“Waafrika na Watanganyika wao ni binadamu kama binadamu wengine wowote duniani, hivyo
wanastahili kukubali kuachana na fedheha ya kutawaliwa na wakoloni kwa kudai uhuru wao.”
Wajibu wao wananchi ni kudai uhuru ili waondokane na fedheha ya kutaliwa na wakoloni, ili wajenge uwezo wao kwa kuwa watu huru wanaojitawala na wafanye mambo yao wenyewe ili kujitegemea.
Mwalimu Nyerere aliwaondoa shaka kwamba licha ya Wazungu kuwachapa viboko hasa wakati wa Vita ya Maji Maji na ndugu zao kufa wakati wa vita hiyo, wasiogope wakati umefika kwao kudai uhuru kwani ni haki yao kuwa huru kama binadamu wengine.
Aliwapa matumaini pia wananchi wengi waliokata tamaa kwamba watajitawalaje wakati hawezi hata kutengeneza hata sindano, Mwalimu Nyerere aliwajenga kiimani kuwa hayo ni matatizo ya muda, akatoa mfano wa kuwa hata Wazungu mfano wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa hawajukua ufundi, jambo muhimu kwao wananchi ni kujifunza na wala si lazima wawe watumwa.
Swali: Katika hotuba ya kuzindua Bunge 1962, Mwalimu Nyerere aliahidi kuwatoa Watanganyika kwenye ujinga, maradhi na umasikini. Je, ni mikakati gani alitumia katika kupambana na maadui hao hadi 1985 alipong’atuka hasa kwa upande wa elimu, afya na kilimo?
Jibu: Lengo la Mwalimu mara tu baada ya kupata uhuru lilikuwa kupambana na maadui hao watatu; ujinga, maradhi na umasikini. Lengo lake lilikuwa kuwakomboa kiafya, kielimu na
kwa kufanya kazi.
Mfano katika suala la afya, kwa kugundua kuwa Watanzania wengi walikuwa wakipoteza maisha
kutokana na kuugua magonjwa mbalimbali hasa malaria kuliko watu wengi walivyokufa wakati
wa vita ya maji maji, Nyerere aliweka mkakati kupambana na maradhi inatakiwa kwa
wananchi ili washughulike na shughuli za kujenga nchi yao.
Hivyo suala la afya ya msingi lilikuwa muhimu kwa raia wa Tanzania, wajitunze kiafya ili
wasipate maradhi ambayo yanakwamisha kushiriki katika shughuli za maendeleo. Katika suala la elimu ya kujitegemea, Mwalimu Nyerere alipigia kelele kwamba Watanzania wanatakiwa kujiendeleza kielimu hasa kwa kupata elimu ya msingi ambayo itolewe bure kwao.
Lakini pia elimu ya maarifa ambayo itawasaidia katika kuishi na itageuza maisha yao, kwani
watazalisha mazao mbalimbali kwa utaalamu zaidi mfano pamba.
Katika suala la kuondoa umasikini, wananchi walitakiwa kufanya kazi hasa za kilimo ambacho hakikuwa tu uti wa mgongo bali kilikuwa ni kiwanda mama cha Watanzania. Hivyo walitakiwa kuzalisha kwa wingi kwa lengo la kutumia wao wenyewe, kuuza na kuweka akiba kwa ajili ya baadaye.
Hivyo, ili mtu azalishe zaidi chakula alitakiwa kuwa na afya njema bila kuugua mara kwa mara
na kwa kuwa mzima aliweza kushiriki katika kazi ambayo ni msingi katika kuondoa umasikini.
Wakati huo wa uongozi wa Mwalimu kulikuwa na kaulimbiu nyingi ikiwamo ya Siasa ni Kilimo,
Uhuru na Kazi, Uhuru ni Kazi, zote hizo zililenga kuwainua wananchi wathamini kilimo ambacho ni uti wa mgongo.
Lengo lilikuwa kuboresha maisha ya wananchi, kutokana na maazio mbalimbali likiwamo la Musoma na la Iringa ambayo hayo na mengine yalilenga k u w a j e n g a wananchi katika
afya na kilimo na katika kuondoa ujinga.
Sera mbalimbali zilizotolewa mfano za Elimu ya Kujitegemea ambazo zilihi m i z a kuwapo kwa
elimu ya m s i n g i . Elimu ambayo kila mtoto mwenye umri wa miaka saba alitakiwa kwenda shuleni na kumaliza darasa la saba akiwa na umri wa miaka 14.
Mwalimu alihimiza kuwa nyenzo ya uhuru ni maendeleo ya elimu kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu.
Kwake, elimu ya msingi ilikuwa kwa ajili ya kila mtu, lakini elimu ya juu kutokana na kuwa gharama kuiendesha, mwalimu alihimiza wapatiwe watu wachache ambao wakihitimu wasaidie kuelimisha wengine mfano madaktari, walimu, mabwana shamba, marubani na wengine wengi.
Hivyo elimu ilikuwa ya msonge, ikiwa na upana katika hatua za awali kwani ilihusisha kila
mtu lakini kadiri inavyozidi kupanda kwenda sekondari, vyuo na vyuo vikuu ni Watanzania
wachache walikuwa wakipata nafasi, kwa lengo la kuwasaidia watu wengine.
Lakini ilitakiwa kuwa bora, kwa wanaostahili na kuwezesha jamii kustahili. Azimio la Musoma, lilihimiza elimu na afya, ambapo kulikuwa na Chuo cha W a u - guzi Vijijini ambao nia ilikuwa kutoa huduma ya afya kwa wananchi wengi vijijini.
Hivyo, hata sekta ya afya ilikuwa ya msonge, kulikuwa na wahudumu wa afya wengi katika
ngazi za zahanati, vituo lakini kulikuwa na madaktari wachache ambao walisoma Muhimbili.
Sera ya Siasa ni Kilimo ya Iringa ilichangia kuweka kanuni kumi za Kilimo Bora, zikiwamo za
kuandaa mashamba mapema, kuweka mbolea, mbegu bora, kupalilia, kuvuna na kuhifadhi
vizuri.
Kilimo hicho kimeendelea kudumishwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni
mikoa maarufu ya Kilimo cha Mahindi ya Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa.
ITAENDELEA JUMATATU…
Habari Leo

No comments:
Post a Comment